Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, August 8, 2017

PEPSI YA ARUSHA NA BULYANKULU ZASHUSHWA DARAJA KWA KUSHINDWA KUSAJILI KWA MTANDAO



TIMU mbili za daraja la pili zimeshushwa daraja kutokana na kushindwa kusajili kwa mfumo wa mtandao TMS
Akizungumza na mtandao huu, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Alfred Lucas alisema timu mbili za Pepsi ya Arusha na Bulyanhullu ya Shinyanga ndio ambazo hazikufanya usajili kati ya timu 64
“Timu za Ligi Kuu, Daraja la Kwanza na Daraja la Pili zilitakiwa kufanya usajili na kuingiza majina ya wachezaji, viongozi wa benchi la ufundi kwenye mfumo wa mtandao wa Transfer Matching System (TMS) lakini Pepsi na Bulyankulu hazikufanya hivyo zimeshushwa daraja,” alisema Lucas
Na kwa msingi huo, timu hizo hazitoshiriki ligi kwa msimu wa 2017/18 na zinashushwa daraja hadi ligi ya wilaya kuanza upya kutafuta nafasi za juu kupanda daraja.
Majina ya timu husika na namna zilivyosajili yamebandikwa katika mbao za matangazo za shirikisho hilo Uwanja wa Karume Dar es Salaam tangu juzi.
Pia Alfred alisema kama kuna dosari TFF imefungua milango ya kupokea pingamizi la usajili wa wachezaji hao kuanzia leo Agosti 8, 2017 hadi Jumatatu Agosti 14, mwaka huu saa 10.00 jioni (16h00).
Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji inatarajiwa kuwa na kikao ama Agosti 16 au 17, mwaka huu kupitia mapingamizi hayo pamoja na usajili wa timu za Ligi Kuu Tanzania Bara. Usajili wa timu za Daraja la Kwanza na Pili, utapitiwa baadaye mwezi huu.

No comments:

Post a Comment