KIUNGO mpya
wa Simba, Haruna Niyonzima amesema hawezi kuongea chochote ila majibu ya
maswali yanayoulizwa juu yake atayaosha uwanjani kuanzia leo.
Niyonzima
aliyasema hayo jana alipozungumza Wandishi wa Habari katika makao makuu ya klabu
hiyo alipokuwa akitambulishwa pamoja na nyota wengine Emmanuel Okwi na Nicholas
Gyan.
Kiungo huyo
ambaye ametokea Yanga baada ya kumaliza mkataba wake alisema kwa sasa yeye ni
mali halali ya Simba na mambo mengine atajibu uwanjani.
“Mimi ni
mchezaji halali wa Simba, sina mengi zaidi ya kuongea kikubwa tukutane
uwanjani,” alisema Niyonzima.
Niyonzima,
Okwi na Gyan wanatarajiwa kuongeza hamasa ya mashabiki wa katika mchezo wa
kirafiki utakaochezwa leo dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda katika Tamasha la Simba
Day.
Kila Agosti
8, klabu ya Simba hufanya tamasha hilo ambalo hutumika kutambulisha kikosi chao
pamoja na kutambulisha jezi.
Niyonzima alikuja jana
na kuanza mazoezi leo asubuhi na kikosi hicho katika Uwanja wa Boko
Veterani, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment