Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, August 7, 2017

KARIA AMWAGA SERA AKANA KUHUSIKA NA NA KUSHIKILIWA KWA MALINZI NA MWESIGWA



MGOMBEA wa nafasi ya Urais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, Wallace Karia amesem hahusiki na kushikiliwa na vyombo vya dola kwa viongozi wa wakuu wa Shirikisho hilo Rais Jamal Malinzi na Katibu Mkuu Mwesigwa Celestine.
Viongozi hao wapo mahabusu kwa zaidi ya mwezi mmoja kwa tuhuma za utakatishaji fedha na matumizi mabaya ya madaraka.
Karia amesema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni zake uliofanyika uwanja wa Taifa ambapo amekataa kuzungumzia suala hilo kwakuwa linashughulikiwa na vyombo vya dola.
Mgombea huyo ambaye ana kaimu nafasi ya urais wa TFF amesema katika wagombea wote sita wa nafasi hiyo yeye ndiye anafaa zaidi kwakuwa analijua vizuri Shirikisho hilo mazuri na mapungufu yake hivyo itakuwa rahisi kufanyika kazi.
“Nilikuwepo kwenye uongozi tangu enzi za FAT, akaja Rais Tenga na baadae uongozi huu unaomaliza muda wake kwahiyo mimi nina uzoefu mkubwa kuliko wenzangu wote.
“Nilikuwa najifunza kwa muda mrefu katika uongozi uliopita na sasa nimeiva nipo tayari kushika hatamu ndani ya TFF, alisema Karia.
Karia ametaja vipaumbele vyake kama akifanikiwa kupata nafasi hiyo kuwa ni nidhamu ya muundo na mfumo wa TFF, Maendeleo ya soka la vijana, Wanawake na ufukweni, Mafunzo na ujenzi wa uwezo, Mapato uwekezaji na nidhamu ya fedha.
Mambo mengine ni miundombinu na vifaa, maboresho ya bodi ya ligi, ushirikiano wa wadau, udhamini na masoko na maboresho ya mashindano.

No comments:

Post a Comment