MGOMBEA
nafasi ya Umakamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Mulamu
Nghambi ameahidi kuinua soka la vijana, wanawake pamoja na kuendeleza miradi ya
michezo nchini.
Nghambi
alisema hayo leo wakati akizindua kampeni zake katika Ukumbi wa habari maelezo Wandishi wa Habari kuhusiana na kile
anachotarajiwa kukifanya pindi akichaguliwa.
Alisema, kwa
muda mrefu maendeleo ya soka la vijana na wanawake kwa ujumla yamekuwa
yakisuasua na yanahitaji mwamko ambao akichaguliwa atahakikisha unakuwapo.
Alisema, ana
uzoefu wa muda mrefu katika kuendeleza soka ambapo mwaka 1999 hadi 2000 alikuwa
meneja msaidizi wa klabu ya Simba na kusha kuja kuwa msaidizi wa masuala ya
kifedha.
Alisema,
amewahi kuwa mjumbe wa kamati ya vijana wa TFF, mjumbe wa kamati ya kusaidia
timu ya taifa ishinde,Mwenyekiti wa chama cha Soka cha Dodoma, Mjumbe wa kamati
ya mabadiliko ya Simba.
Kuhusiana na
kanuni iliyowekwa na Baraza la Michezo la Taifa(BMT) inayozuia mtu kuwa na
kofia mbili katika mchezo wa soka, Nghambi alisema kuwa ataachia nafasi ya uenyekiti
akishinda nafasi yake hiyo ya Umakamu wa Rais.
Pia aligusia
uhusiano wake na klabu ya Simba hasa katika kuangalia ni kwa kiasi gani
hautoweza kuwa na mgongano wa kimaslahi iwapo akichaguliwa kushika wadhifa huo
wa Umakamu, alisema kuwa yeye ni mwadilifu na hatochanganya mambo hayo mawili.
Alisema,
atafanya kazi na kila mtu, kila timu, kila kundi, kila klabu na kila chama ili
mradi wawe na malengo ya kuendeleza soka la hapa nchini.
Alisema
atahakikisha kuwa anaimarisha mifumo bora zaidi ya uchumi wa klabu na vyama vya
michezo ikiwa pamoja na kuinua ligi daraja la kwanza, la pili hasa katika
kuwatafutia wadhamini.
Alikosoa
mfumo wa sasa wa uendeshwaji wa soka kwa kuwa umegubikwa na uzamani hasa
kutokana na kuwa kila Mkoa una dira yake inayofuata katika kuendesha soka.
Alisema,
atahakikisha kuwa anajenga dira moja ya kitaifa itakayoziwezesha klabu za Soka
kuwaendeleza wachezaji na wanafunzi wa soka kupata soko la uhakika ndani na nje
ya nchini.
No comments:
Post a Comment