Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, August 7, 2017

SIMBU AANZA KURUDISHA HESHIMA YA RIADHA TANZANIA



MWANARIADHA Alphonce Simbu ameitoa Tanzania kimasomaso kwenye michuano ya riadha ya dunia ya London Marathon baada ya kushika nafasi ya tatu.

Kwa mujibu wa habari kwenye mitandao mbalimbali ya kimataifa jana, mwanariadha huyo amejishindia medali ya Shaba baada ya kushika kwake nafasi hiyo ambapo alionesha umahiri mkubwa katika kufukuza upepo kwenye mashindano hayo.

Nusura ashike nafasi ya pili iliyochukuliwa na mwanariadha Tamirat Tola wa Ethiopia, kwani mkongwe huyo wa Ethiopia alimshinda Simbu kwa sekunde mbili tu.

Simbu ameshika nafasi ya tatu baada ya kumaliza kwa muda wa saa 2: 09:51 huku mshindi wa kwanza ambaye ni Mkenya, Geofrey Kirui akishinda kwa saa 2:08: 22.

Simbu amemshinda Muingereza Callum Hawkins aliyeshika nafasi ya 4 kwa kumaliza kwa aaa 2:10:17, huku  Gideon Kipkater raia wa Kenya akishika nafasi ya 5 kwa kumaliza kwa saa 2: 10: 56.

Simbu, mwenyeji wa Arusha na kiongozi wa timu ya riadha iliyoshiriki michuano hiyo, amewakilisha vema kwa kushika nafasi hiyo ambayo hakuna Mtanzania aliyewahi kushinda kwenye michuano hiyo.

Simbu alishika nafasi ya tano kwenye michezo ya Olimpiki Rio de Janeiro, Brazil mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu alishika nafasi ya kwanza kwenye Mumbay Marathon.

Kwa upande wake Katibu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania, Filbert Bayi alimpongeza mwanariadha huyo na kusema hatua hiyo imetokana na maandalizi mazuri.

Alisema, kitendo cha mwanariadha huyo kupewa Sh milioni 1 kila mwezi na DSTv ni mchango mkubwa kwake na kwamba kuajiriwa kwake na Jeshi la Kujenga Taifa, JKT,  pia kumesaidia kumwezesha kufanya vema kwa kuwa imempunguzia mawazo ya kifamilia.

Bayi alikiri kuwa michuano hii aliyoshiriki Simbu ni mikubwa iliyojaa kila aina ya ushindani na kuwapongeza washiriki wote kutokea Tanzania.

Katika mashindano hayo aliyeshika nafasi ya 6 ni Daniel Meucci kutoka Italia, huku Yohana Ghebregergis kutoka Eritrea akishika nafasi ya saba.  Aliyeshika nafasi ya nane ni Daniel Wonjin kutoka Kenya.

No comments:

Post a Comment