Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, August 6, 2017

GADIEL MICHAEL MALI YA YANGA SASAImage result for GADIEL MICHAEL
Azam FC imetangaza kumruhusu mchezaji Gadiel Michael kujiunga na Yanga baada ya Klabu  zote kufikia makubaliano.
Jafar Idd alisema, Yanga wametakiwa kulipa nusu ya dau ambalo walitakiwa kulipa awali kwa ajili ya kumsajili Gadiel ambaye mkataba wake na Azam utamalizika Disemba mwaka huu.
“Leo mchana tulikuwa na mazungumzo na viongozi wa Yanga, alikuja Nyika na viongozi wenzie. Sisi tuliwapa dau letu wakaona ni kubwana sana lakini kukawa na dhana imejengeka kwamba tumewapa dau kubwa ili washindwe,” alisema Jafar Idd
“Tuliwaita leo waje walipe nusu ya kile ambacho tuliwaambia walipe awali ili tufanikishe lengo lao kwa mchezaji wanaemtaka.”
“Kwa hiyo tumekubaliana kisheria kabisa na sisi kama Azam tumewapa mchezaji Gadiel Michael ambae inaonekana kwa muda mrefu walikuwa wanamtaka maana inaonekana walikuwa wana hamu nae.”
“Azam tayaritumeshampa mchezaji barua ya kuondoka (release latter) kwenda Yanga kwa ajili ya msimu ujao.”