Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, June 8, 2017

TAIFA STARS KARATA MUHIMU JUMAMOSI



 Image result for taifa stars logo
MCHEZO wa kwanza wa Kundi L kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na Lesotho ‘Mamba’ utachezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam Jumamosi kuanzia Saa 2:00 usiku.
Akizungumza na wandishi wa habari leo, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Nchini, (TFF) Alfred Lucas alisema  sababu za mchezo huo kufanyika Uwanja wa klabu ya Azam ni kutokana na Uwanja wa Taifa kuwa katika matengenezo madogo.
Alfred amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi Jumamosi Azam Complex, kuisapoti timu yao ili iweze kufanya vizuri.
Taifa Stars itaingiaa kwenye mchezo huo ikitoka kwenye kambi ya wiki moja mjini Alexandria, Misri.
Nahodha Mbwana Ally Samatta hakuwepo Misri lakini ameshaungana na wenzake Dar es Salaam akitokea Ubelgiji ambako anachezea klabu ya KRC Genk.
Kiungo wa DC Tenerife ya Hispania, Farid Mussa na mshambuliaji wa AFC Eskilstuna ya Denmark, Thomas Ulimwengu wao walikuwepo Misri na wako tayari kwa mchezo wa keshokutwa.

No comments:

Post a Comment