Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, June 8, 2017

YANGA YAAGA MASHINDANO YA SPORTPESA








MABINGWA wa Tanzania, Yanga imeaga mashindano ya SportPesa Super Cup baada ya kutolewa kwa penalti 4-2 na AFC Leopards baada ya kutoka suluhu ndani ya dakika 90 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo, Leopards itamenyana na Gor Mahia ambayo iliifunga Nakuru All Stars mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa jioni uwanja wa Uhuru.
Mshindi katika fainali hizo atajinyakulia dola za kimarekani 30,000 zaidi ya Sh. Milioni 65 na nafasi ya kucheza na Everton ya England Julai 13.
Kipa namba moja wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’ aliokoa mkwaju wa Marselas Ingotsi, lakini mlinda mlango wa AFC Leopards, Dennis Shika naye akacheza mikwaju ya Said Mussa na Said Juma ‘Makapu’.
Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na kiungo mshambuliaji Mzambia, Obrey Chira ndiyo pekee walifunga penalti za Yanga, wakati Bernard Mango, Allan Katerega, Duncan Otieno na Dennis Shika wakafunga za AFC Leopards.
Katika dakika 90 za mchezo, timu zote zilimiliki mpira sawa, ingawa hakukuwa na mashambulizi ya kushitua.
Kikosi cha Yanga kilikuwa: Deogratius Munishi ‘Dida’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Juma Abdul, Mohammed Ally, Andrew Vincent ‘Dante’, Pato Ngonyani/Babu Ally Seif dk 61, Juma Mahadhi, Maka Edward/Said Juma dk 76, Obrey Chirwa, Yussuf Mhilu/Samuel Greyson dk 53 na Emmanuel Martin/Said Mussa dk 56.
AFC Leopards: Dennis Shika, Otieno Ian, Marcus Abwao/Mike Kibwage dk 88, Joshua Mawira, Salim Abdallah, Duncan Otieno, Mango Bernard, Allan Kateregga, Vincent Obura, Yakubu Ramadhani na Gilbert Fiamento/Marselas Ingotsi dk 56.