Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, June 8, 2017

AZAM TV KUONESHA NDONDO CUP, MAKUNDI KUPANGWA KESHO

Mkurugenzi wa Azam TV, Tido Muhando (kulia) akishikana mikono na mwanzilishi wa Ndondo Cup, Shafii Dauda baada ya kutia saini makubaliano ya kuonesha mubashara mashindano hayo ambayo yanafanyika mkoa wa Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam, (DRFA) Almas Kasongo (Picha na Rahel Pallangyo)




Kituo cha Televisheni cha Azam kimeingia makubaliano ya mwaka mmoja ya kuonesha mubashara mashindano ya Ndondo hatua ya makundi ambayo yanachezwa katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya kutia saini makubaliano hayo, Mkurugenzi wa Azam TV, Tido Muhando alisema wameamua kuingia makubaliano na Clouds Media ili kuwaonesha watu ambao hawawezi kufika katika viwanja kushuhudia mashindano hayo.
“Tunawaahidi Clouds na watanzania wote kuwa tutafanya kazi nzuri kwani sisi ndio kituo bora nchini kwa urushaji wa matangazo hasa soka hilo halina ubishi,” alisema Tido.
Naye Mratibu wa Ndondo Cup Shafii Dauda aliwashukuru Azam Media kuwa sehemu yao katika kuendesha mashindano hayo kwa miaka minne mfufulizo.
“Lengo la mashindano ni kutengeneza daraja kwa vijana wenye vipaji ili waonekana na baadae wasajiliwe na timu za madaraja ya juu hivyo tunaishukuru Azam Media kuwa sehemu yetu kufanikisha ndoto za vijana,” alisema Shafii.
Kwa upande wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam, Mwenyekiti wake, Almas Kasongo aliishukuru Azam Media na Clouds Media kwa kusaidia kuendeleza michezo Dar es Salaam.
“Tunafurahi kuona soka likichezwa katika mkoa wetu kwani mnasaidia kutekeleza moja ya majukumu yetu hivyo nawaahidi mashindano haya yatasimamiwa kwa weledi mkubwa,” alisema Kasongo.
Droo ya makundi ya mashindano hayo inatarajiwa kuchezeshwa leo katika viwanja vya Escape One, Kinondoni ambapo timu 32 zitakuwa kwenye bakuli moja.
Timu hizo ni Vituka FC, Twiga International, Kigoma Kombaini, Stimtosha, Tandavamba, Black Six, Ukwamani, Ndanda Investment, Miami, Mpakani Kombaini na Kibo Kombaini.
Vijana rangers, Goroka FC, Burudani, Polisi DSM College, Faru jeuri, Boom FC, Temeke Market, Temeke Squad, Tabata United, Misosi, Keko Furniture na Buguruni United.
Zingine ni Goms United, Kigogo Kombaini, Wauza matairi, Shelaton, Makuburi, Kibada One, Kauzu FC, Mlalakuwa Rangers na Madiba FC.

No comments:

Post a Comment