Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, May 6, 2017

YANGA YEREJEA KILELENI LIGI KUUUSHINDI wa mabao 2-0 ambao Yanga iliupata katika mchezo wake wa kiporo Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Prisons Uwanja wa Taifa  Dar es Salaam, umeifanya timu hiyo ianze kupiga honi za kukaribia ubingwa.

Yanga imefikisha pointi 59 na kushika usukani wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiiengua Simba yenye pointi 59 iliyokuwa inaongoza ligi kabla ya matokeo ya mechi hiyo ya Yanga, ambapo Yanga ina uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Simba yenyewe imecheza mechi 27 ikitarajiwa kushuka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kesho kucheza na African Lyon katika mchezo wa raundi ya 28 ya ligi hiyo. Yanga imecheza mechi 26.

Kutokana na Yanga kuwa mechi moja ya kiporo kabla ya mechi ya Simba, huku pia ikiongoza ligi hiyo, ina nafasi kubwa ya kutetea ubingwa, kwani ikishinda mchezo wake wa kiporo itaizidi Simba pointi tatu.

Yanga ikishinda michezo yake minne iliyobaki kabla ya kumaliza ligi hiyo itafikisha pointi 72, wakati Simba yenyewe ikishinda michezo yake mitatu iliyobaki itafikisha pointi 69.

Kwa upande wa Simba yenyewe inaombea Yanga itoke sare michezo angalau miwili ama itoke sare mmoja na kufungwa mmoja, huku yenyewe ikitakiwa kushinda michezo yake yote ili kutwaa ubingwa huo.

Simba ikishinda kesho dhidi ya African Lyon itarejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa tofauti ya pointi tatu dhidi ya Yanga, lakini itakuwa inaizidi Yanga michezo michezo miwili.

Katika mchezo wa leo timu hizo zilienda mapumziko zikiwa hazijafungana, kabla ya mambo kubadilika dakika 20 za mwisho, hasa baada ya kuingia Haruna Niyonzima badala ya Said Juma ‘Makapu’ dakika ya 65.

Yanga ilipata bao la kuongoza dakika ya 71 mfungaji akiwa Amis Tambwe akiunganisha kwa kichwa krosi ya Juma Abdul, likiwa ni bao la 10 kwa Tambwe kwenye ligi hiyo msimu huu.
Dakika nne baadaye , Obrey Chirwa aliiandikia Yanga bao la pili kwa kichwa akiunganisha mpira wa Tambwe. Bao hilo pia lilikuwa la 10 kwa Tambwe msimu huu.

Yanga: Benno Kakolanya, Hassan Kessy/Juma Abdul,  Haji Mwinyi, Kelvin Yondan, Vincent Bossou, Said Juma ‘Makapu’/Haruna Niyonzima, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Obrey Chirwa/Matheo Anthony na Geoffrey Mwashiuya.

Prisons; Aaron Kalambo, Benjamin Asukile, Michael Ismail, James Mwasote, Nurdin Chona, Jumanne Elfadhil, Salum Kimenya, Mohammed Samatta/Nchinjay Kazungu, Victor Hangaya/Kassim Hamisi, Lambert Sibiyanka na Meshack Suleiman.

Wakati huohuo, Simba leo itakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Lyon, ambapo katika mchezo wa kwanza msimu huu, Lyon ilishinda bao 1-0.

Ni wazi Simba haitakubali kupoteza mchezo huo na kufifisha ndoto zake za ubingwa, huku pia Lyon inayoshika nafasi ya 11 katika msimamo ikiwa na pointi 31 itataka kushinda ili kujihakikishia kubaki Ligi Kuu msimu ujao.