Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, May 16, 2017

YANGA YAIADHIBU TOTO AFRICAN TAIFA NA KUKARIBIA UBINGWA







HATA kama hautaki, Yanga ndio mabingwa wa msimu wa 2016/17 baada ya kuifunga Toto Africans ya Mwanza kwa bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Baada ya ushindi huo Yanga imefikisha jumla ya pointi 68, ambazo zinaweza kufikia wa Simba, lakini endapo tu Yanga watafungwa katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Mbao FC mjini Mwanza Jumamosi.
Pamoja na Simba kuwa na uwezekano wa kuifikia Yanga kwa pointi, lakini ni ndoto kwa timu hiyo kuifunga Mwadui kwa zaidi ya mabao 12.
Yanga ina mabao 57 ya kufunga na kufungwa 13, hivyo ina wastani wa mabao 44 wakati Simba imefunga mabao 48 na imefungwa 16, hivyo ina wastani wa mabao 32 imepitwa na Yanga kwa mabao 12.
Pamoja na katika soka lolote linawezekana, lakini timu kufunga mabao 12 katika mchezo mmoja ni jambo lisilowezekana kwani tangu msimu huu uanze, hakuna timu iliyowahi kufunga zaidi ya mabao hayo.
Katika mechi 29, ambazo Simba tayari imeshacheza, haijawahi kushinda zaidi ya mabao matano, hivyo timu hiyo tayari msimu huu imeshindwa kutwaa taji hilo.
Katika mchezo huo wa jana, Amis Tambwe ndiye aliyeiwezesha Yanga kuondoka na pointi zote tatu na kujihakikishia ubingwa mara ya tatu mfululizo baada ya kufunga bao katika dakika ya 82 baada ya kupata pasi kutoka kwa Juma Abdul.
Vikosi vilikuwa:-
Yanga:Beno Kakolanya, Vicent Bossou, Juma Mahadhi/Kaseke, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Kelvin Yondani, Thaban Kamusoko, Haruna Niyonzima, Obrey Chirwa na Amis Tambwe.
Toto Africans: Lucajo Lerient, David Kissu, Mohamed Soud, Hamimu Abdu, Ramadhani Malima, Yusuph Mlipili, Carlos Protas, Juvenary Pastory/Waziri Ramadhani, Hussein Kasanga na Waziri Junior.
Mechi zingine za kufunga pazia la Ligi Kuu zitakazofanyika Jumamosi ni Azam FC ataikaribisha Kagera Sugar, huku Majimaji atakuwa mwenyeji wa Mbeya City, Stand United dhidi ya Ruvu Shooting, Mtibwa Sugar na Toto Africans, Prisons dhidi ya African Lyon na Ndanda itacheza na JKT Ruvu ambayo tayari imshashuka daraja.



No comments:

Post a Comment