Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, May 16, 2017

SERENGETI BOYS YACHANGIWA SHILINGI MILIONI 12WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe jana alipokea kiasi cha sh milioni 12 kwa ajili ya timu ya taifa ya vijana ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys.

Serengeti Boys iko nchini Gabon, ambako inashiriki mashindano ya 12 ya Mataifa ya Afrika, Afcon 2017, ambapo juzi ilianza kwa suluhu dhidi ya mabingwa watetezi Mali.

Fedha hizo ni sh milioni 10 kutoka kwa DStv na mil. 1 ya Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru),  ambazo zilikabidhiwa  na Mkurugenzi wa Maelezo, Hassan Abbas.

Pia Misa Tanzania nao walikabidhi sh milioni 1 ambayo ilitolewa na mwenyekiti wake Salome Kitomari.

Waziri Mwakyembe aliwashukuru wote waliotoa michango hiyo na kuwataka wadau kuendelea kuichangia timu hiyo, ambayo inawakilisha nchi katika mashindano hayo ya Afcon 2017.

Aidha, Mwakyembe alisema kuwa wote walioichangia timu hiyo atawatangaza katika magazeti ya Serikali ya Daily News na HabariLeo kama alivyoahidi awali kuwa kila anayechangia atatangazwa.