Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, May 16, 2017

WADAU WAOMBWA KUENDELEA KUICHANGIA SERENGETI BOYS



WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe ameyataka makampuni na taasisi mbalimbali nchini kujitosa kudhamini michezo.

Waziri Mwakyembe aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa kuiaga timu ya Azania inayokwenda kushiriki fainali za Kombe la Standard chartered zitakazofanyika wiki ijayo kwenye Uwanja wa Anfield, England chini ya udhamini wa benki ya Standard Chartered.

Alisema kujitokeza kudhamini kutasaidia  kuhamasisha na kuinua michezo nchini.

Aidha, aliitaka timu hiyo kucheza kwa jitihada zote na kuhakiisha inarejea na Kombe na anaamini kwa ubora iliyonayo, watarudi na ubingwa.

“Ni wakati wenu wa kwenda kuionesha dunia nzima kama mnaweza na mafanikio yenu yatawatia moyo na vijana wengine," alisema.

Timu hiyo ambayo ni mabingwa wa Afrika Mashariki, ikiwa Uingereza inatarajia kupambana na timu kutoka Botswana, Nigeria, HongKong, Korea, India na wenyeji Uingereza.

Awali, Mjumbe wa bodi ya benki ya Standard Chartered Balozi Ammi Mpungwe alisema ni mara ya kwanza kwa timu ya Tanzania kushiriki mashindano hayo na anaimani na timu hiyo itatumia vyema fursa hiyo kuhakikisha wanarudi na ushindi.

No comments:

Post a Comment