KOCHA wa
Manchester United, Jose Mourinho amesema kwamba nahodha wa klabu hiyo, Wayne
Rooney, ana wakati mgumu sana kisoka.
Mourinho
ambaye amekuwa akimbania Rooney kwa kumwacha nje kabisa ya kikosi au kumweka
benchi, amesema kwamba mchezaji huyo anaelekea kwenye siku za mwisho za kucheza
soka ya ushindani, hivyo anatakiwa kuwa makini kisaikolojia.
Rooney
anaweza kuondoka United kiangazi hiki ikiwa hataridhika na idadi ya mechi au
dakika anazopangiwa kucheza, na Everton alikozaliwa wanamtaka, lakini pia Ligi
Kuu ya China inaweza kumpata na kumpatia kiasi kikubwa cha fedha.
Imedaiwa pia
kwamba Mourinho alikuwa akipanga kumkosesha ‘send off’ leo watakapomaliza Ligi
Kuu ya England (EPL) kwa kucheza na Crystal Palace, kwani anadaiwa kutaka
kumwaga uwanjani makinda.
Mourinho
alipoulizwa iwapo Rooney angecheza leo alisema: “Sijui. Alicheza dakika 90
kwenye mechi iliyopita (dhidi ya Southampton) kwa hiyo labda hapana. Nitachukua
wachezaji watatu au wanne wa kikosi cha kwanza na kila mmoja atacheza nusu ya
mechi ili kukipa kikosi uzoefu kidogo, lakini nataka kuwaacha wachezaji kwa
ajili ya Jumatano (fainali ya Ligi ya Europa dhidi ya Ajax).
Mourinho
amejumuisha chipukizi 10 kwenye kikosi cha wachezaji 18 wa kuivaa Palace, nao
ni Axel Tuanzebe, Tim Fosu-Mensah, Joel Pereira, Kieran O’Hara, Demetri
Mitchell, Scott McTominay, Josh Harrop, Matty Willock, Angel Gomes na Zak
Dearnley.
Kadhalika
amesema kwamba Zlatan Ibrahimovic, pamoja na majeruhi wengine, Marcos Rojo,
Luke Shaw na Ashley Young, watasafiri na timu kwenda Stockholm kwa ajili ya
mechi hiyo ya Jumatano.
No comments:
Post a Comment