Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, May 21, 2017

KARIM BENZEMA AMGEUZIA KIBAO VALBUENA



MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Karim Benzema amemgeuzia kibao mchezaji wa Lyon na timu ya Taifa ya Ufaransa, Mathieu Valbuena, akidai alimwekea uongo juu ya tuhuma za kumhusisha na mkanda wa video za ngono.
Benzema (29) aliyekuja kutemwa kikosi cha Ufaransa, alidaiwa kuchonga mpango wa kupata kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa Valbuena (32) anayechezea Lyon, akidai kuna mshirika wake alikuwa na kanda za video za ngono za Valbuena na ikiwa hangetoa fedha hizo, basi picha zingetundikwa mtandaoni na kumwaibisha.
Wakati suala hilo likiendelea kwa utata kwa muda sasa huku ukweli ukiwa haujulikani, Benzema ameibukia Madrid, Hispania na kudai kwamba rafiki yake huyo wa zamani ni mwongo na mfitini aliyeamua kumharibia heshima yake mbele ya jamii na kwamba suala lote hilo lilitungwa na Valbuena.
Benzema akasema kwamba uongo wa Valbuena unamfanya achanganyikiwe kiakili, huku akibaki nje ya kikosi cha timu ya taifa, akisema ni sawa na mtu aliyetupwa kwenye matope.
Benzema alidaiwa kutumia vipande vya kanda vilivyo kwenye simu ya mkononi kumtishia Valbuena, akashitakiwa kwa usaliti.
Desemba mwaka jana, korti iliyopo Versailles ilikataa maombi ya Benzema ya kutaka kusitisha mwendelezo wa shauri hilo ambapo alishitakiwa kwa kula njama za usaliti tangu Novemba 2015.
“Huyu jamaa ana tatizo fulani …hii yote ni hadithi yake. Yaani ninapomsikia akisema eti yupo tayari kucheza nami tena nashangaa, maana alshasema mie ni mchafu, nilimtishia na kumtia hofu.
“Sasa anasema eti asingefungua kesi kama angejua kwamba nilihusika. Kwa zaidi ya mwaka mmoja unusu mie ndiye adui yake mkubwa zaidi, kijana mbaya, mhuni, natakiwa kuadhiniwa, kutupwa kwenye matope, jina langu na la familia yamechafuliwa,” anasema Benzema.
Mfaransa huyo anasema kwamba hajamuona rafiki yake wa karibu, Karim Zenati, anayedaiwa kuwa na kanda hizo, tangu kashfa hiyo iibuliwe, kwa sababu alizuiwa kumwona, wakati ndiye ‘best’ wake na anasema yupo tayari kwenda jela kwa kosa ambalo hakulifanya.

No comments:

Post a Comment