Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, April 2, 2017

SERENGETI BOYS YAIPIGA BURUNDI 5-0, KESHO KUCHEZA NA GHANA TAIFAWachezaji wa Timu ya Serengeti Boys wakimpongeza mfungaji wao wa bao la pili Ibrahim Abdallah2-0

TIMU ya Taifa ya soka ya Vijana waliochini ya miaka 17 ‘Serengeti boys’kesho inashuka uwanjani kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Ghana utakaochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo maalumu kwa ajili ya kuiaga timu hiyo ambayo inakwenda kuweka kambi nchini Morocco kwa ajili ya kujianda na fainali za Afrika za vijana, nchini Gabon unakuja ikiwa ni takribani siku nne tangu iifunge timu ya taifa ya Burundi kwa mabao 5-0.
Serengeti boys ilicheza na Burundi kwenye Uwanja wa Kaitaba Kagera na kufanikiwa kuifunga timu hiyo kwenye mchezo wa kwanza mabao 3-0 na mchezo wa pili uliochezwa juzi mabao 2-0.
Akizungumza jijini, Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF), Alfred Lucas alisema Ghana ambao nao wanashiriki fainali za vijana iliwasili nchini tangu Ijumaa usiku.
“Mchezo huu ndio vijana wetu wanaotumia kama sehemu ya kuwaaga watanzania kwani tunatarajia kiongozi mzito wa serikali atakuwepo ili kukabidhi bendera,” alisema Lucas.
Aprili 5, Serengeti boys inatarajiwa kusafiri kwenda Morocco kwa ajili ya kambi na ikiwa Morocco itacheza michezo ya kimataifa ya kirafiki na Cameroon na Misri na Mei 6 itakwenda Gabon tayari kwa mashindano kwani wanatakiwa wawe wamewasili Mei 7.

Serengeti Boys imepangwa kundi ‘B’ pamoja na mabingwa watetezi Mali, Niger na Angola ambapo fainali hizo zinajuisha mataifa nane ya Afrika, endapo Serengeti itafuzu nusu fainali itakuwa imekata tiketi ya kucheza fainali za dunia za vijana zitakazofanyika India, Novemba.