Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, April 5, 2017

KUIONA YANGA NA MC ALGER NI 5000KIINGILIO cha chini katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya  Yanga na MC Alger ya Algeria ni Sh. 5,000.
Mchezo unatarajiwa kuchezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na viingilio vingine vitakuwa Sh. 20,000 kwa VIP B na C na 30,000 kwa VIP A.  
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa alisema maandalizi ya mchezo yanaendelea vizuri.
Mkwasa amesema kwamba wapinzani wao, MC Alger wanatarajiwa kuwasili Alhamisi Saa 3:30 usiku mjini Dar es Salaam.
Tayari Shirikisho ya Soka Afrika (CAF), limetaja marefa wa Rwanda na Guinea watakaochezesha mechi mbili za mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga SC na MC Alger ya Algeria ambao ni Louis Hakizimana akisaidiwa na Theogene Ndagijimana na Jean Bosco Niyitegeka wote kutoka Rwanda.
Mchezo wa marudiano Aprili 14 nchini Algeria utachezeshwa na marefa wa Guinea, ambao ni Yakhouba Keita, Aboubacar Doumbouya na Mamady Tere na mshindi wa jumla atafuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka huu.
Mwaka jana pia Yanga ilitolewa katika Ligi ya Mabingwa na kuangukia kwenye kapu la kuwania hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho ambako ilifuzu baada ya kuitoa Sagrada Esperanca ya Angola. 
Yanga SC imeangukia Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Zanaco Uwanja wa Taifa wa Mashujaa, Lusaka nchini Zambia ikitoka kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.