Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, April 6, 2017

JOSE MOURINHO AMSIFIA LUKE SHAW


Meneja wa Manchester United amemsifia beki wake Luke Shaw ambae Jana aliingizwa Kipindi cha Pili na kuzua Bao la kusawazisha la Dakika za Majeruhi la Timu yake walipotoka 1-1 na Everton Uwanjani Old Trafford.
Majuzi Mourinho alimponda Shaw kwa kutojituma na huku wengi wakidhani zama za Mchezaji huyo zimekwisha, Meneja huyo akamjumuisha kwenye Kikosi cha kuivaa Everton.
Jana Shaw, mwenye Miaka 21, alianza Benchi na kuingizwa Kipindi cha Pili kumbadili Ashley Young ambapo Shuti lake lililolenga Goli lilishikwa na Beki wa Everton Ashley Williams na kuzaa Penati ambayo Zlatan Ibrahimovic aliifunga katika Dakika ya 94 na kuipa Man United Sare ya 1-1.
Akiongea baada ya Mechi hiyo Mourinho alieleza: "Nishamwambia haya. Amecheza vizuri kwa kutumia mwili wake na akili zangu. Alikuwa mbele karibu yangu na nilimwamulia kila kitu. Inabidi sasa afanye bidii afanye maamuzi mwenyewe. Ni Mchezaji mzuri mwenye kipaji. Mchango wake ulikuwa mzuri na kuifanya Timu icheze vyema!"
Mbali ya Shaw, Mourinho pia alilalamikia baadhi ya maamuzi ya Mechi yao na Everton ya kukataliwa Bao zao 2 kwa Ofsaidi tata hasa lile la Ibrahimovic huku Paul Pogba na Ander Herrera wakipiga Posti.