Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, April 6, 2017

LIVERPOOL YAPIGWA ''STOP'' KUSAINI CHIPUKIZI MIAKA 2, FAINI £100,000


Liverpool imepigwa Faini Pauni Laki 1 na kufungiwa kusaini Chipukizi baada ya kukiri kuvunja Sheria za Ligi Kuu England, EPL, zinazolinda na kudhibiti Usajili wa Makinda hao. Liverpool wamepatikana na Hatia ya kumrubuni Chipukizi aliekuwa Klabuni Stoke City na sasa hawaruhusiwi kusaini Chipukizi yeyote kwa Mwaka Mmoja na Kifungo cha Mwaka Mmoja unaofuata kusimamishwa na kuwepo kwenye Angalizo kwa Miaka Mitatu ili kosa hilo lisirudiwe.
Wasimamizi wa EPL wameridhika kuwa Liverpool ilijaribu kumrubuni Kijana wa Miaka 12 aliyesajiliwa na Stoke City kwa kutoa Ofa ya kumlipia Ada za Shule na kuwalipa Wazazi wake ili aihame kwao bila maridhiano kwa Klabu hizo mbili kitu ambacho kilikuwa kinyume cha taratibu.

EPL imesema Liverpool wamekiri Kosa lao na wamekubali Adhabu zao.