Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, March 16, 2017

ZANZIBAR MWANACHAMA WA KUDUMU CAF

Zanzibar
Kilio cha muda mrefu cha Zanzibar kupewa hadhi ya mwanachama kamili wa CAF kimeisha kwa kwa furaha baada ya Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo kupitisha ombi la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) la Zanzibar kuwa mwanachama kamili wa CAF.
Wajumbe wa mkutano wa CAF hii leo wamepiga kura suala la Zanzibar na kupitisha ajenda ya visiwa hivyo vya Tanzania kuwa mwanachama kamili.
Awali kikao cha Kamati ya Utendaji kilichokaa Januari 12, mwaka huu kiliamua kupitisha ombi hilo kuwa moja ya ajenda za Mkutano Mkuu wa CAF ulioanza jana mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Ajenda ya uanachama wa Zanzibar imepata idadi ya kura theluthi mbili yaani 2/3 ya wanachama wote na hivyo visiwa hivyo kutangazwa kuwa mwanachama mpya kamili wa CAF ambako itakuwa na haki mbalimbali kama wanachama wengine 54.
Haki hizo ni pamoja na kushiriki michuano yote inayoandaliwa na kusimamiwa na CAF na hii ni pamoja na Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon), fainali za Afrika Wanawake (Awcon), fainali za vijana (Afcon U-17 na 20) na pia kuhudhuria mikutano mbalimbali ya CAF kama mwanachama kamili, kupokea na kusimamia kozi mbalimbali za CAF.
Pia Zanzibar itakuwa na fursa ya kupiga kura katika masuala muhimu ya CAF tofauti na zamani ilipokuwa inaambulia fursa ya klabu zake zinazoshika nafasi ya juu katika Ligi Kuu ya Zanzibar kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.