SAFARI ya Yanga kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa
Afrika imepata hitilafu baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya
Zanaco ya Zambia katika mechi ya raundi ya kwanza iliyochezwa kwenye Uwanja wa
Taifa Dar es Salaam.
Matokeo hayo yanailazimisha Yanga kupata ushindi wowote
katika mechi ya marudiano itakayochezwa mjini Lusaka mwishoni mwa wiki ijayo
ili kusonga mbele.
Simon Msuva alikuwa wa kwanza kuiandikia Yanga bao
la kuongoza katika dakika ya 38 akiunganisha pasi ya Justin Zullu kabla ya
kuujaza mpira wavuni.
Zanaco ilipata bao lake la kusawazisha katika dakika
ya 78 likifungwa na Atram Kwame baada ya kuunganisha vema pasi ya Ernest Mbwewe
na kuujaza mpira wavuni.
Katika mechi hiyo wageni walitawala katika vipindi
vyote na walionekana kukamilika kila idara hali iliyoisumbua Yanga na kuonyesha
kwamba wanatakiwa kujiandaa na kuwa makini katika mechi ya marudiano kwani
wachezaji wake walionekana kuwahi kuchoka.
Yanga ilianza kulishambulia lako la Zanaco dakika ya
11 kupitia kwa kiungo wake Thaban Kamusoko ambaye hata hivyo nafasi nzuri
aliyopata alishindwa kuitumia. Dakika moja baadae Zanaco pia ilikosa bao
kupitia kwa mchezaji wake Saith Sakala lakini shuti lake lilipanguliwa kiustadi
na kipa wa Yanga Deogratius Munishi ‘Dida’.
Augustino Mulenga nusura aifungie Zanaco bao katika
dakika ya 18 lakini akiwa kwenye nafasi nzuri alipiga shuti dhaifu lililoishia
mikononi mwa Dida.
Yanga: Deogratius Munishi ‘Dida’, Hassan Kessy,
Mwinyi Haji, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Vincent Bossou, Kevin Yondan, Simon
Msuva, Justin Zulu, Donald Ngoma/Emmanuel Martin dk58, Thabani Kamusoko/Juma
Mahadhi dk60 na Obrey Chirwa.
Zanaco: Racha Kola, Ziyo Kola, Zimiseleni Moyo,
Chongo Chirwa, Saith Sakala/Kennedy Musonda dk69, Taonga Mbwemya, Richard
Kasonde, Attram Kwame, Augustine Mulenga, Ernest Mbewe na George Chilufya.
No comments:
Post a Comment