Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, March 28, 2017

Watanzania Walivyoambulia Patupu Riadha Uganda

WANARIADHA wa timu ya Taifa ya Tanzania walioshiriki mashindano ya kimataifa ya mbio za Nyika za Dunia ‘IAAF World Cross Country Marathon’ hawajaambulia medali hata moja kwa upande wa wanawake na wanaume.
Mashindano hayo yanayoandaliwa na shirikisho la riadha duniani (IAAF) yamefanyika katika viwanja vya Kololo jijini Kampala ambapo nchi 60 zimeshiriki huku jumla ya wanariadha 557 wakitimuliana vumbi.
Tanzania yenyewe imewakilishwa na wanariadha Failuna Abdi, Magdalena Shauri, Angelina Daniel, Maylelina Issa, Sara Ramadhan na Siata Kalinga kwa upande wa wanawake waliokimbia mbio za kilomita nane.
Upande wa wanaume waliokimbia mbio za kilomita 10 ni Emmanuel Giniki, Gabriel Gerald, Fabian Joseph, Josephat Joshua, Simon Naali na Michael Sylvester.

Upande wa mbio za ‘Mixed Relay’ za kilomita mbili iliwakilishwa na Faraja Damas, Sicilia Panga, Jackline Sakilu na Marco Monko ambao pia hawakuambulia kitu.
Upande wa wanariadha chini ya miaka 20 wanaume ni walikuwa ni Francis Damiano, Ramadhan Juma, Elisha Dosla, Joshua Sule, Anthiny Dosla na Yohana Elisante wakati wanawake ni Elizabeth Boniphace, Amina Mohamed, Shamima Ramadhan na Asha Salum ambao wamekimbia mbio za kilomita sita.
Timu hiyo ambayo iliingia jijini Kampala usiku wa kuamkia jana Jumamosi inatarajia kugeuza kesho Jumatatu asubuhi kwa usafiri wa barabara.