Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, March 25, 2017

SAMATTA AWAPA RAHA WATANZANIA LEO, TAIFA STARS IKISHINDA 2-0


NAHODHA wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars Mbwana Samatta  leo ameng'aa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam baada ya kufunga mabao yote mawili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Botswana.
Mechi hiyo ya kirafiki ya kimataifa ilikuwa ya kwanza kwa kocha mpya wa timu hiyo Salum Mayanga lakini pia ilikuwa ya kwanza kushuhudiwa na Waziri mpya wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe ambaye jana alikuwepo uwanjani.
Mwakyembe amechukua nafasi ya Nape Nnauye kufuatia mabadiliko yaliyofanywa na rais Dk John Magufuli Alhamis ya wiki hii.
Nahodha Samatta, anayecheza KR Genk ya Ubelgiji  aliuchangamsha mchezo huo katika dakika ya pili tu baada ya kufunga bao la kuongoza kwa kuunganisha pasi ya Shizza Kichuya na kuujaza mpira wavuni.
Katika kipindi cha kwanza cha mechi hiyo Stars ilionekana kufanya mshambulizi ya mara kwa mara huku wachezaji wake wakikosa mabao kadhaa ikiwemo Ibrahim Ajib katika dakika ya 7 ambapo alitengenezewa mpira na Samatta lakini akashindwa kufunga baada ya kuupiga vibaya.
Dakika ya 33 nusura Botswana ipate bao la kusawazisha kupitia kwa Lebogang Disele lakini akiwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga, mpira wake ukagonga mwamba na kuwahiwa na mabeki wa Stars.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu lakini Stars bado ilionekana kuwa vizuri zaidi ya wapinzani wao ambapo washambuliaji wa Stars pia walikosa mabao mengi kabla Samatta hajafunga bao la pili katika dakika ya 87.
Samatta alifunga bao hilo kwa mpira wa adhabu ndogo nje ya 18 iliyotolewa na mwamuzi Elly Sasii wa Dar es Salaam baada ya kufanyiwa madhambi na mchezaji wa Botswana.
Mechi hiyo ni ya kirafiki kujiandaa na michuano ya kimataifa, ambapo keshokutwa timu itakayochezwa mechi za kuwania kufuzu kombe la mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) itacheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Burundi.
Mechi ya jana ilikuwa ya kwanza kwa kocha Mayanja tangu apewe nafasi hiyo baada ya kujiuzulu kwa Charles Mkwasa.
Stars: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jnr’, Erasto Nyoni, Abdi Banda, Himid Mao, Simon Msuva/Said Ndemla, Frank Domayo/Muzamil Yassin, Mbwana Samatta, Ibrahim Ajib, Shiza Kichuya/Farid Mussa.
Botswana: Kabelo Dambe, Tapiwa Gadibolae, Kaone Vanderwesthuizem, Lesenya  Ramoraka, Lesego Galenamotlhale, Ofentse Nato, Lebogang Ditsele, Omaaatla Kebatho, Mosha Gaolaolwe, Thacng Sesenyi, Mogakolod Ngele.