![](http://dewjiblog.co.tz/wp-content/uploads/2016/05/tff.jpg)
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi wake wa Fedha na Utawala, marehemu Edgar Masoud.
Edgar Masoud aliyefariki dunia jana jioni Machi 27, 2017 aliugua ghafla juzi Jumapili akiwa kanisani kabla ya kukimbizwa Hospitali ya Bochi iliyoko Mbezi kwa Msuguri ambako alikutwa na mauti akipatiwa matibabu.
No comments:
Post a Comment