Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, April 1, 2017

YANGA YAREJEA KILELENI, JE ITADUMU KWA SAA 24?


Azam FC wameshindwa kuendeleza ubabe wao wa kuinyima ushindi Yanga baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ulliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
Yanga imepata ushindi leo ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 4-0 waliyofungwa na Azam kwenye mashindano ya Mapinduzi yaliyofanyika Zanzibar
Bao pekee la Yanga limefungwa na mshambuliaji Obrey Chirwa baada ya kunasa mpira uliokuwa uliorudishwa kwa kipa na Erasto Nyoni na kumtoka beki Yakubu Mohamed na kuachia shuti kali lililomshinda golikipa na kuingia wavuni
Kwa ushindi huo Yanga ambayo ndio mabingwa watetezi inarejea kileleni baada ya kufikisha pointi 56 pointi moja mbele ya Simba ambao kesho watakuwa na kibarua cha kuwakabili Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba Kagera.
Mechi ya leo imeongeza idadi ya majeruhi kwenye vikosi vya timu zote kwani Yanga kiungo Justine Zulu aliumia na kutolewa uwanjani kwa msaada wa machela na kuwahishwa zahati iliyopo uwanjani kwa ajili ya matibabu zaidi.
Kwa upande wao Azam, walimkosa mshambuliaji wao Yahaya Mohamed ambaye alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumiana kusababisha mchezo kusimama mara kadhaa ili atibiwe lakini baadae alishindwa kuendelea na mchezo na kulazimika kutoka.
Tangu mwaka 2014, Yanga ilikuwa haijapata ushindi dhidi ya Azamna timu hizo zilikutana mara sita kabla ya leo huku michezo mitano zikiwa zimetoka sare na Azam wakashinda mechi moja.