Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, February 24, 2017

UAMUZI WA KIKAO CHA SAA 72



Kikao cha Bodi ya Kusimamia na Kuendesha Ligi, kiliketi mwanzoni mwa wiki hii na kufanya tathmini ya mambo mbalimbali yaliyotokea kwenye michezo mbalimbali ya mpira wa miguu kwa michuano yote – Ligi Kuu ya Vodacom, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili.



Haya haya ndiyo yaliyojiti katika kila mchezo.



Mechi namba 170 (Stand United FC vs Majimaji). Majimaji iliwasilisha malalamiko kuwa chumba chao kubadilishia nguo (changing room) kilipuliziwa na timu pinzani dawa ambayo ni sumu, hivyo kushindwa kukitumia wakati wa mapumziko.
Klabu ya Stand United FC pamoja na Meneja wa Uwanja waandikiwe barua kuwa vitendo hivyo vikiendelea kujitokeza uwanja huo utafungiwa kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom.

Msimamizi wa Kituo aandikie taarifa yake (report) kuhusu tukio hilo. Pia Daktari wa Uwanja, Dk. Abel Kimuntu awasilishe taarifa yake ya kitaalamu kuhusu suala hilo, vilevile Meneja wa Uwanja huo, Meja mstaafu Mohamed Ndaro naye awasilishe taarifa yake kuhusu tuhuma hizo za kumwaga dawa kwenye vyumba.

Mechi namba 173 (Ruvu Shooting vs Azam). Klabu ya Ruvu Shooting iandikiwe barua kuhusu ubovu wa uwanja wake eneo la kuchezea (pitch) ambapo kuna mashimo, hivyo wafanyie marekebisho.

Ligi Daraja la Kwanza

Mechi namba 49 (Polisi Morogoro vs Kinondoni Municipal Council FC). Klabu ya Polisi Morogoro imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa kuchelewa kufika uwanjani kwa dakika 20, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(9) ya Ligi Daraja la Kwanza. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(48) ya Ligi Daraja la Kwanza.

Mechi namba 52 (Mbeya Warriors vs Njombe Mji). Mchezaji Boniface S. Nyagawa wa Mbeya Warriors amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kutoa lugha ya matusi kwa Mwamuzi Msaidizi Namba Moja, tukio lililosababisha atolewe kwenye benchi kwa kadi nyekundu. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 37(7).

Mechi namba 49 (Polisi Mara vs Singida United FC). Mwamuzi Msaidizi Namba Moja, Enock Mwanyonga, na Mwamuzi Msaidizi Namba Mbili, Abdulaziz Ally wameondolewa kwenye orodha ya waamuzi wa Ligi Daraja la Kwanza baada ya kushindwa kumudu mchezo huo.

Uamuzi huo umefanywa kwa mujibu wa Kanuni ya 38(1a) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.

Mechi namba 56 (Singida United vs Alliance Schools FC). Mwamuzi Msaidizi Namba Moja, Omari Miyala, na Mwamuzi Msaidizi Namba Mbili, Innocent Mwalutanile wamefungiwa miaka miwili kwa kushindwa kumudu mchezo huo. Uamuzi dhidi yao umezingatia Kanuni ya 38(1a) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.

Naye Kamishna Hamisi Kambi ameondolewa kwenye orodha ya Makamishna wa Ligi Daraja la Kwanza kwa kushindwa kutoa taarifa ya mchezo huo kwa usahihi. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 39(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Kamishna/Mtathmini Waamuzi.

Klabu ya Alliance Schools FC imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kugoma kuinbia kwenye chumba vya kubadilishia (changing room), hivyo kusababisha timu yako ikaguliwe kwenye gari. Adhabu imezingatia Kanuni ya 14(48) ya Ligi Daraja la Kwanza.

Ligi Daraja la Pili

Mechi namba 27 (Bulyanhulu FC vs Mashujaa). Klabu ya Bulyanhulu FC imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) baada ya timu yake kuchelewa kufika kwenye kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting). Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili.

Waamuzi wa mechi hiyo; Mwamuzi Elikana E. Mhoja (Mwanza), Mwamuzi Msaidizi Namba Moja, John Mrisho (Mwanza), na Mwamuzi Msaidizi Namba Mbili, Mukhusin I. Abdallah wa Mwanza wameondolewa kwenye orodha ya waamuzi kwa kushindwa kumudu mchezo huo. Uamuzi dhidi yao umezingatia Kanuni ya 38(1a) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.

Pia timu ya Bulyanhulu FC ilichelewa kufika kwenye kikao hicho katika mechi namba 28 dhidi ya Milambo FC iliyofanyika kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, mjini Tabora.

Mechi namba 30 (Mawenzi Market vs Sabasaba United). Klabu ya Mawenzi Market imepigwa faini ya sh. 100,000 (laki moja) kwa kufika kwenye kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting) ikiwa na maofisa wawili tu badala ya wanne, na pia kutokuwa na vifaa vya mchezo. Adhabu dhidi ya klabu ya Mawenzi Market imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili.

Mchezaji Awadh Ahmed wa Sabasaba United amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kumsukuma Mwamuzi na kugoma kutoka uwanjani baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 37(7) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.

AJENDA 79/MSC/2017- MALALAMIKO YA ALLIANCE SCHOOLS

Malalamiko ya Alliance Schools FC kupinga matokeo ya mechi yake dhidi ya Singida United kwa madai mabao mawili waliyofungwa si halali, na mchezo huo urudiwe kwenye uwanja huru (neutral) yametupwa.

Msingi wa kutupa malalamiko hayo ni kuwa matokeo ya uwanjani hayawezi kubadilishwa kwa sababu ya kupinga mabao yaliyofungwa

No comments:

Post a Comment