Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, February 24, 2017

AZAM SPORTS FEDERATION CUP KUENDELEA LEO


Baada ya Simba kutangulia robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) yaani Azam Sports Federation Cup kwa kuifunga African Lyon kwa bao 1-0, mechi nyingine za kuwania nafasi hiyo zitaanza kuchezwa kesho Ijumaa Februari 24, mwaka huu.

Simba iliilaza African Lyon katika mchezo wa hatua ya 16 bora uliofanyika Februari 16, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Michezo ya leo kwa mujibu wa ratiba inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), itakuwa ni kati ya Madini FC ya Arusha na JKT Ruvu ya Pwani watakaocheza kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wakati Kagera Sugar itacheza Stand United ya Shinyanga Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Mechi nyingine itakuwa ni kati ya The Mighty Elephant ya Ruvuma na Ndanda FC ya Mtwara zitakazopambana kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea ilihali Azam na Mtibwa Sugar watacheza Chamanzi –Mbagala, Dar es Salaam. Michezo yote itaanza saa 10.00 jioni.

Jumapili Februari 26, mwaka huu timu ya Mbao FC itacheza na Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Tanzania Prisons itacheza na Mbeya City zote za Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Machi 7, mwaka huu Young Africans SC itacheza na Kiluvya United kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam

No comments:

Post a Comment