Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, February 27, 2017

MWANARIADHA AFARIKI KWENYE MBIO ZA KILIMANJARO MARATHON 
Mwanariadha, Charles Maroa kutoka nchini Kenya amefikwa na mauti katika hospitali ya KCMC mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro, baada ya kuanguka katika geti la viwanja vya Ushirika wakati alipokuwa akielekea kumaliza mbio za nusu Marathon za Kilimanjaro zilizofanyika jana Februari 26.
Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, RPC Raymond Mtafungwa alisema kuwa Mwanariadha huyo alikutwa na umauti huo jana majira ya saa tano asubuhi katika hospitali la KCMC mjini Moshi baada ya kuanguka.
"Tumepokea taarifa za kifo cha Mwanariadha huyo alietambulika kwa jina la Charles Maroa,ambaye ni raia wa Kenya (Mkurya), baada ya kukumbwa na hali hiyo alikimbizwa hospitali ya KCMC kupatiwa huduma ya kwanza baada ya kuanguka ghafla katika geti kuu la kuingia katika viwanja vya Ushirika hapa mjini Moshi wakati alipokuwa akielekea kumaliza mbio za nusu Marathon za Kilimanjaro na tunaendelea na uchunguzi kujua nini kilitokea mpaka kuelekea kifo chake" alisema.
Mwili wa Mwanariadha huyo umehifadhiwa katika hospitali ya KCMC mjini Moshi.