Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, February 15, 2017

ANTONIO CONTE AMJIBU MOURINHO KIMYAKIMYA


Antonio Conte amesema hapendi 'mzaha'wa Jose Mourinho baada ya Meneja huyo wa Manchester United kudai Chelsea ambao ni Vinara wa EPL, Ligi Kuu England, hawawezi kukamatika kileleni kwa sababu ni timu 'inayojihami.
Hivi sasa Chelsea wana pointi 10 mbele ya timu ya pili Tottenham baada jana kutoka 1-1 na Burnley huko Turf Moor.
Mourinho, ambae anasifika kwa kuchota akili za Mameneja wapinzani na kuwavuruga, juzi alidai Chelsea haiwezi kuteleza kutoka kileleni kwa vile 'wanajihami mno' na kushinda kwa kutumia 'kaunta ataki'.
Jana Meneja wa Chelsea Antonio Conte alijibu mapigo kwa kusema: "Hiyo ni hadaa yake. Nina uzoefu kuelewa hilo!"
Mara nyingi Mourinho amekuwa akikwaruzana na Mameneja wenzake kutokana na vijembe vyake vya kuwapandisha munkari ili kushinda vita ya kisaikolojia na muhanga mkuu wa mashambulizi hayo huko nyuma akiwa Arsene Wenger wa Arsenal.

Hata hivyo Conte amegoma kuburutwa kwenye vita hiyo na kujibu: "Sipendi kujibu kuhusu Makocha wengine!" 

EPL – Ligi Kuu England
RATIBA:
Jumatatu Februari 13

2300 Bournemouth v Manchester City
Jumamosi Februari 25
1800 Chelsea v Swansea City
1800 Crystal Palace v Middlesbrough
1800 Everton v Sunderland
1800 Hull City v Burnley
Southampton v Arsenal [IMEAHIRISHWA]
1800 West Bromwich Albion v Bournemouth
2030 Watford v West Ham United
Jumapili Februari 26
1630 Tottenham Hotspur v Stoke City
Manchester City v Manchester United[IMEAHIRISHWA]
Jumatatu Februari 27
2300 Leicester City v Liverpool
Jumamosi Machi 4
1530 Manchester United v Bournemouth
1800 Leicester City v Hull City
1800 Stoke City v Middlesbrough
1800 Swansea City v Burnley
1800 Watford v Southampton
1800 West Bromwich Albion v Crystal Palace
2030 Liverpool v Arsenal
Jumapili Machi 5
1630 Tottenham Hotspur v Everton
1900 Sunderland v Manchester City
Jumatatu Machi 6
2300 West Ham United v Chelsea

No comments:

Post a Comment