Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, January 14, 2017

KOCHA AFRICAN LYON ATAMBA KUIFUNGA MBAO FC



KOCHA wa African Lyon, Charles Otieno amejigamba kuifunga Mbao FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Akizungumza kwa njia ya simu, Otieno alisema anajua Mbao ni timu nzuri lakini pia wao ni wavuri ndio maana wanacheza ligi kuu hivyo anatarajia kurudi na pointi tatu.
“Naijua Mbao FC ni timu nzuri na watacheza nyumbani na kuongezewa nguvu na mashabiki wao lakini maandalizi ambayo nimefanya kipindi cha wiki mbili yananipa jeuri ya kusema nitachukua pointi tatu ugenini,” alisema Otieno
Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani kwani timu hizi zimeachana kwa pointi moja, African Lyon inashika nafasi ya 11 ikiwa na pointi 20 na Mbao wana pointi 19 kwenye nafasi ya 12.
Ligi Kuu inatarajia kuendelea Januari 16, 2017 ambapo Tanzania Prisons itakuwa mgeni wa Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Januari 17, 2017, Majimaji ya Songea itakuwa wenyeji wa mabingwa watetezi  Yanga katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma.
Mtibwa Sugar itakacheza na Simba, Januari 18, 2017 kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro wakati Azam itakuwa mwenyeji wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Mchezo wa Azam na Mbeya City utaanza saa 1.00 usiku lakini michezo mingine itaanza saa 10.00 jioni lengo likiwa ni kutoa nafasi kwa mashabiki kushuhudia mechi nyingi kupitia Kituo cha Televisheni cha Azam  ambao ni wadhamini wenza wa ligi kuu.

No comments:

Post a Comment