Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, January 10, 2017

CRISTIANO RONALDO MCHEZAJI BORA DUNIANI NA KOCHA BORA NI CLAUDIO RANIERI


HAFLA ya FIFA ya kutunuku Tuzo za FIFA za Ubora Duniani kwa Mwaka 2016 zimefanyika Usiku huu huko Zurich, Uswisi na Cristiano Ronaldo kuibuka ndio Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani.
Akitwaa Tuzo hii, Ronaldo, anaechezea Real Madrid na Nchi yake Portugal, aliwashinda kwa Kura Lionel Messi na Antoine Griezmann.

Ronaldo pia alitwaa, mapema Mwezi Desemba, Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani kwa 2016, Ballon d’Or, inayotolewa na Jarida la France, France Football, Tuzo ambayo kabla ya hapo, kwa Miaka 6, iliunganishwa na FIFA na kuitwa FIFA Ballon d’Or, lakini kuanzia safari hii wametengana.
Kwa upande wa Kinamama, Mchezaji Bora ni Carli Lloyd wa USA.

Kocha Bora Duniani kwa Wanaume ni Claudio Ranieri baada ya kuiwezesha Leicester City, bila kutegemewa, kutwaa Ubingwa wa England kwa mara ya kwanza katika Historia yao.
Nae Mohd Faiz Subri wa Penang, Malaysia ndie alitwaa Tuzo ya Puskas ya Goli Bora la Mwaka. Kwenye Tuzo ya Mashabiki, Mashabiki wa Timu za Liverpool na Borussia Dortmund, kwa pamoja, wameshinda Tuzo hii kwa tukio la kuimba wote ‘Wimbo wa Taifa wa Liverpool’ -'You'll Never Walk Alone'- Uwanjani Anfield kabla ya Mechi yao ya Robo Fainali ya UEFA EUROPA LIGI Msimu uliopita. FIFA TUZO ZA UBORA – WAGOMBEA NA MSHINDI:
MCHEZAJI BORA WANAUME:
-Wagombea:
Cristiano Ronaldo, Antoine Griezmann, Lionel Messi
-Mshindi: Cristiano Ronaldo

MCHEZAJI BORA WANAWAKE:
-Wagombea: Melanie Behringer, Carli Lloyd, Marta
-Mshindi: Carli Lloyd wa USA.
KOCHA BORA WANAUME:
-Wagombea: Claudio Ranieri, Fernando Santos, Zinedine Zidane
-Mshindi: Claudio Ranieri wa Mabingwa wa England Leicester City

KOCHA BORA WANAWAKE:
-Wagombea: Jill Ellis, Silvia Neid, Pia Sundhage
-Mshindi: Silvia Neid [Germany]

GOLI BORA [Tuzo ya Puskas]:
-Wagombea: Marlone, Daniuska Rodriguez, Mohd Faiz Subri
-Mshindi: Mohd Faiz Subri wa Penang, Malaysia.
 

Tuzo hii inatokana na Kura za Mashabiki Duniani kote.
TUZO TOKA KWA MASHABIKI:

-Wagombea: Mashabiki wa Den Haag, Borussia Dortmund & Liverpool na Iceland.
-Mshindi: Mashabiki wa Borussia Dortmund & Liverpool

TUZO YA UCHEZAJI WA HAKI
-Mshindi:
Atletico Nacional ya Colombia
FIFA FIFPro World11 2016 – Kikosi Bora cha Mwaka 2016:
-Kipa: Neur
-Mabeki: Alves, Pique, Ramos, Marcelo
-Viungo: Modric, Kroos, Iniesta
-Mafowadi: Suarez, Ronaldo, Messi

No comments:

Post a Comment