Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, December 27, 2016

YANGA KIBARUANI KESHO, LWANDAMINA ASITISHA MAZOEZI

LIGI Kuu Tanzania Bara inatarajia kuendelea kesho katika viwanja viwili  ambapo mabingwa watetezi Yanga watacheza na Ndanda kwenye Uwanja wa Uhuru huku Mtibwa wakiwakaribisha Majimaji Uwanja wa Manungu Turiani Morogoro.
Yanga wanashuka dimbani wakiwa na kumbukumbu ya  sare 1-1 ya African Lyon waliyoipata mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja huo wa Uhuru.
Mtibwa wao walishinda wa mabao 2-0 waliopata kwa Ndanda FC ugenini hivyo inaweza ikawa chachu kufanya vizuri mchezo wa leo.
Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina ameendelea na mazoezi na kikosi chake na mshambuliaji Donald Ngoma amefanya mazoezi na wenzake baada ya kukosa mchezo uliopita akitumikia adhabu ya kadi tatu za njano.
Kwenye mazoezi yanayofanyika katika Uwanja wa Uhuru, wachezaji wa Yanga wameonekana kujinoa vilivyo kwani wanataka ushindi kutoka kwa Ndanda FC ambapo mechi ya awali walitoka sare Mtwara.
Leo Yanga wakiwa katikati ya mazoezi, timu ya Ndanda walifika wakitaka kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Uhuru ndipo Lwandamina alisitisha mazoezi na kuwaruhusu wachezaji kwenda kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kesho.
Endapo Yanga watashinda mchezo wa leo watafikisha pointi 40 na kubaki kwenye nafasi ya pili na nafasi itaendelea kubaki kwa Simba yenye p[ointi 41.
Mtibwa  wamejizatiti kushinda mchezo baada ya kutoka na ushindi ugenini dhidi ya Ndanda na wamesema kuwa raundi hii ya pili itakuwa ni ya ushindi tu kwao hawatakubali kupoteza mchezo wowote.