Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, December 19, 2016

SIMBA YARUDI KWENYE NAFASI YAKE Simba wameonyesha kuwa wao si watu wa 'mchezo mchezo' baada ya kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu kwa kuifunga Ndanda mabao 2-0 kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Simba ambao juzi walishushwa kileleni na Yanga wenye pointi 36  walipata mabao yao kupitia kwa Mzamiru Yassin dakika ya 63 na Mohamed Ibrahim dakika ya 81 hivyo kujihakikishia ushindi uliowarejesha tena kileleni kwa kufikisha pointi 38.


Simba walionyesha uwezo mkubwa katika eneo la kiungo ambapo Mzamiru aliyeingia badala ya James Kotei aliyeumia alishirikiana vema na Jonas Mkude katika eneo la kati huku kuingia kwa Said Ndemla kukiwavuruga Wanakuchele ambao hawakuwa na cha kufanya ili kuwazuia Simba wasipate mabao.


Kipa mpya Daniel Agyei alionyesha umahiri kwa kuokoa hatari kadhaa na kufanikiwa kuwaondoa patupu washambuliaji wa Ndanda walioongozwa na Omari Mponda