Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, December 19, 2016

ZAHORO PAZI AKUTANA NA KUTETA NA RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI

Image may contain: 3 people, people sitting

MSHAMBULIAJI wa Mbeya City, Zahoro Pazi leo amekutana na Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi kujadiliana juu ya kuzuiwa kwa ITC yake na klabu ya FC Lupopo ya DR Congo.

Wiki iliyopita Zahoro, alituma ujumbe kwa Malinzi aone namna ya kumsaidia kupatikana  ITC ili aweze kuichezea Mbeya City.

Zahoro aliweka wazi kuwa ITC yake ilitolewa na Boniface Wambura (Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya ligi) bila idhini yake huku akidai hajawahi kusaini mkataba na Lupopo kwa sababu makubaliano yao hayakufikiwa.
Kikao hicho kimefanyika Break Point, Kinondoni na kuhudhuriwa pia baba mzazi wa Zahoro, Idd Pazi na mwakilishi wa Mbeya City, Mohamed Mashango.

Habari za ndani ya kikao hicho zinasema Malinzi ameahidi kushughulikia tatizo hilo na ametoa muda wa siku saba ITC yake itakuwa imepatikana.


Zahoro alianza kushughulikia ITC hiyo miaka miwili iliyopita lakini juhudi zake ziligonga mwamba kwa sababu alikosa nguvu kutoka TFF huku Lupopo wakisisitiza kuwa ni lazima arejeshe pesa aliyochukuwa wakati anasaini mkataba huo hewa.


Zahoro hajacheza ligi kwa miaka miwili ingawa Polisi Moro pamoja na African Sports ziliwahi kuhitaji huduma yake lakini alishindwa kucheza