Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, December 19, 2016

CRISTIANO RONALDO AIBEBESHA REAL UBINGWA WA DUNIA KWA BAO 4-2


Mchezaji Bora Duniani Cristiano Ronaldo Leo amepiga Bao 3 na kuwawezesha Real Madrid kutwaa Kombe la Ubingwa kwenye Fainali ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu huko Yokohama International Stadium Nchini Japan kwa kuwachapa Wenyeji wao Kashima Antlers 4-2 kwenye Mechi iliyokwenda Dakika 120 baada ya Sare 2-2 katika Dakika 90.
Real walitangulia kufunga kupitia Karim Benzema na Kashima kujibu kwa Bao kabla Haftaimu na jingine mara tu baada ya Haftaimu zote zikifungwa na Gaku Shibasaki.

Real walisawazisha kwa Penati iliyofungwa na Ronaldo ambayo ilitolewa baada ya Lucas Vazquez kuangushwa kwenye Boksi na Shuto Yamamoto.

Hadi Dakika 90 kwisha Bao zilikuwa 2-2 na Mechi kwenda Dakika 30 za Nyongeza na ndipo Ronaldo alipopiga Bao 2 zaidi na kuwapa Real Uningwa wa Dunia kwa ushindi wa 4-2.

Ushindi huu wa Leo umeendeleza wimbi la Real kutofungwa katika Mechi 37.

Ushindi huu wa Real umeletwa kwa mchango mkubwa wa Ronaldo ambae mapema Wiki hii alizoa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani, Ballon d'Or, na pia kuukamilisha Mwaka mwema kwake ambao yeye ndie alifunga Penati ya Ushindi kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI Mwezi Mei na kuwapa Ubingwa Real wakati pia Mwezi Julai, akiwa Nahodha wa Portugal, aliiongoza Nchi yake kutwaa EURO 2016, Ubingwa wa Mataifa ya Ulaya.

Pia Hetitriki ya Leo imemuweka kuwa Mchezaji wa Kwanza kabisa kupiga Bao 3 katika Fainali ya Kombe la Dunia kwa Klabu.

Hii pia ni mara ya 3 kwa Ronaldo kutwaa Kombe hili na mara nyingine alitwaa akiwa na Manchester United Mwaka 2008 na Real Mwaka 2014.

Vile vile, Ronaldo ameweka Rekodi ya kufunga Goli nyingi, Bao 5, kwenye Fainali za Mashindano haya akifungana na Mchezaji mwingine.


MAGOLI:
Real Madrid 4

-9’ Karim Benzema
-60’, 98 & 104’ Cristiano Ronaldo [Bao la Pili kwa Penati]
Kashima Antlets 2
-44’ & 52’ Gaku Shibasaki

VIKOSI:
Real Madrid:
Navas; Carvajal, Ramos, Varane, Marcelo; Casemiro, Modric, Kroos; Vazquez, Ronaldo, Karim Benzema

Kashima Antlers: Sogahata; Daigo, Shoji, Ueda, Nagaki; Yamamoto, Endo, Mitsuo, Shibasaki, Shoma; Kanazaki

REFA Janny Sikazwe [Zambia]

FIFA KOMBE LA DUNIA KWA KLABU
Ratiba/Matokeo
Alhamisi Des 8

Kashima Antlers 2 Auckland City 1

Jumapili Des 11
Robo Fainali
Jeonbuk Hyundai Motors 1 América 2
Mamelodi Sundowns 0 Kashima Antlers 2

Jumatano Des 14
Mshindi wa 5

Jeonbuk Hyundai Motors 4 Mamelodi Sundowns 1

Nusu Fainali
Atlético Nacional 0 Kashima Antlers 3

Alhamisi Des 15

Club América 0 Real Madrid 2

Jumapili Des 18
Mshindi wa 3

Atletico Nacional 2 Club America 2 [Penati 4-3]

Fainali

Kashima Antlers 2 Real Madrid 2 [4-2, Real Mabingwa baada ya Dakika 120]