Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, December 2, 2016

Serikali yairuhusu Yanga kutumia Uwanja wa Taifa

01-1
Serikali imesaini Mkataba na Klabu ya Yanga kutumia Uwanja Mkuu wa Taifa pamoja na Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya michezo yote ya Kimataifa pamoja na michezo ya Ligi Kuu ya ndani.
Mkataba huo umesainiwa jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel kwa niaba ya Serikali na Kaimu Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga Baraka Deusdedit kwa niaba ya Klabu ya Yanga.
Katika Mkataba huo, Klabu ya Yanga imeruhusiwa kutumia viwanja hivyo kama viwanja vyake vya nyumbani kwa sharti la kuvitunza viwanja hivyo wakati wote wanapovitumia.
Miongoni mwa masharti hayo ni kutunza viwanja, mali na vifaa vyote vilivyopo katika viwanja hivyo, na endapo kutatokea uharibifu wowote utakaofanywa na wachezaji ama mashabiki, Klabu hiyo itawajibika kubeba gharama za matengenezo yote yatakayotokana na uharibifu huo.
Aidha, Klabu ya Yanga inaweza kutumia viwanja hivyo kwa mazoezi ya kujianadaa na mechi zinazowakabili.

No comments:

Post a Comment