Katika tukio hilo, Mwenyekiti wa muda wa TBN, Bwana Joachim Mushi amepongeza benki ya NMB kwa kuweza kudhamini tukio hilo muhimu na la kihistoria kwani litasaidia wana blogger kwa ujumla kuweza kukutana pamoja na kujifunza kile ambacho wanapaswa kuwahabarisha Umma kupitia blog zao.
“Tunawapongeza benki ya NMB kwa udhamini huu na tunawaomba sana waendelee kutudhamini kwani kazi iliyopo mbele yetu kwa sasa ni kutoa elimu sahihi kwa wenzetu ambao watajumuika katika mkutano huu utakaofanyika siku mbili yaani 5 na 6 Desemba,2016. Kwa washiriki takribani 150 kutoka Tanzania nzima ambapo pia tukio hilo litafuatiwa na mkutano mkuu kwa wanachama hai wa TBN na kujadili mambo mbalimbali,” alieleza Joachim Mushi.
Ofisa Uhusiano wa NMB, Doris Kilale amesema kuwa wataendelea kushirikiana na Tanzania Bloggers Network-TBN kwani inaamini kufanya hivyo ni moja ya njia ya kufikisha ujumbe kwa jamii hasa kupitia mitandao ya kijamii.
“NMB imekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na wadau wa habari mbalimbali na sasa tunashirikiana na TBN na tumeweza kutoa kiasi cha Shilingi milioni 10 kwa ajili ya mkutano wao wa mwaka utakaofanyika 5 na 6 Desemba mwaka huuna. Pia kama munavyofahamu kuwa NMB ipo karibu yako hivyo kupitia mitandao ya kijamii na Blog itaendelea kufikisha habari zetu kwa jamii kwa wigo mpana zaidi.” alieleza Ofisa Uhusiano huyo, Doris Kilale.
Mkutano huo unatarajia kufanyika jijini Dar es Salaam hiyo 5 na 6 Desemba katika ukumbi wa wa mikutano wa makao makuu ya jengo la Golden Jubilee PSPF.
Aidha, mbali na Benki ya NMB kuwa wadhamini wakuu katika tukio hilo, pia wadhamini wengine ni pamoja na NHIF,SBL, PSPF na Coca Cola ambao wote kwa pamoja wamejitokeza kufanikisha katika tukio hilo.
Mwenyekiti
wa muda wa TBN, Bwana Joachim Mushi akizungumza na waandishi wa Habari
(Hawapo pichani) wakati wa tukio hilo la kukabidhiwa mfano wa cheki ya
Tsh. Milioni 10 kutoka kwa Benki ya NMB. Anayemfuatia ni Ofisa Uhusiano
wa NMB, Doris Kilale.
Ofisa
Uhusiano wa NMB, Doris Kilale akizungumza na waandishi wa Habari wakati
wa tukio hilo la kukabidhi mfano wa cheki ya Tsh. Milioni 10 kwa TBN.
Ofisa
Uhusiano wa NMB, Doris Kilale akikabidhi mfano wa cheki ya Tsh. Milioni
10 kwa Mwenyekiti wa muda wa TBN, Bwana Joachim Mushi. Wengine
wanaoshuhudia ni maafisa kitoka NMB na TBN.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakichukua habari katika tukio hilo la NMB na TBN kukabidhiana cheki
Mkutano huo
Meza kuu maafisa wa NMB na TBN katika mkutano huo. wakati wa kukabidhiwa cheki ya mfano ya Tsh. milioni 10.
PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE
No comments:
Post a Comment