Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, December 2, 2016

BARAZA LA WADHAMINI LAMWANGUKIA MAKONDA

BARAZA la wadhamini wa Simba limemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kusimamisha mkutano wa dharura wa mabadiliko ya katiba uliopangwa kufanyika Disemba 11 kutokana na wao kutoshirikishwa chochote kama wenye mali.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa baraza hilo, Mzee Hamisi Kilomoni alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana akasema inaweza kuleta mpasuko ambao unaweza kuleta madhara kiusalama.
“Mkutano uliopita mliona Mwenyekiti Aveva akitolewa chini ya usalama wa askari hali iliyoonesha kuwa usalama ulikuwa mdogo hivyo tunaomba mkutano wa Disemba 11, usifanyike hadi wanachama wahakikiwe,” alisema Mzee Kilomoni

Pia Kilomoni alisema wamepokea barua kutoka kwa wanachama wa wakilalamikia mkutano huo ambapo nakala za barua zimefika hadi kwa Rais John Magufuli, Waziri Mkuu, Waziri wa Michezo, Baraza la Michezo (BMT) pamoja na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) hivyo kwa kuangalia kwa kina wanaiomba serikali kusimamisha mkutano huo.

"Hapa kuna barua nyingi kutoka kwa wanachama kuomba kusitisha mkutano huo, mpaka kufikia kupeleka barua kwa Rais wa nchi ujue hilo sio suala dogo sisi kama wenye klabu tumeamua kumuomba Mkuu wa mkoa kuusimamisha ili isije ikatokea balaa zaidi," alisema Kilomoni.
Aidha Mzee Kilomoni alisema bado yeye yupo kwenye orodha ya wadhamini wanne wa klabu hiyo baada ya kupinga kuenguliwa kwenye mkutano mkuu wa wanachama uliofanyika Agosti mwaka 2014.

Kilomoni alithibitisha kwa kuonesha barua kutoka RITA iliyotolewa Agosti 12 mwaka huu ikianisha majina ya wadhamini wa klabu ya Simba ambao ni Abdul Wahab Abas, Ally Sykes (marehemu), Ramesh Patel na yeye mwenyewe.