Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, December 23, 2016

MKHITARYAN MCHEZAJI BORA WA MWAKA KWA MARA YA 6 MFULULIZO


KIUNGO wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan amepata tuzo ya sita mfululizo ya mchezaji Bora wa mwaka kwa nchi ya Armenia.
Hii ni tuzo yake ya saba tangu avuke umri wa miaka 20 na kumfanya awe kwenye rekodi za mastaa wa dunia waliopata tuzo ya aina hiyo mara nyingi 
Anaeongoza kwa tuzo aina hii kwa nchi yake ni mchezaji mwenzake Mkhitaryan wa Man United, Zlatan Ibrahimovic, ambaye amechukua mara 11.
Wengine wanaomkimbiza Ibrahimovic ni wachezaji toka Finland, Sami Hyypia, aliyetwaa mara tisa na Jari Litmanen, mara nane, na Kipa wa Czech Republic, Petr Cech mara nane.

Lakini hao wote wamestaafu timu za Taifa wakati Mkhitaryan bado anacheza akikaribiwa kwa karibu na akina Gareth Bale wa Wales na David Alaba wa Austria, wote wakiwa na Tuzo sita kila mmoja.

Wengine waliowahi kutwaa tuzo sita enzi zao ni Andriy Shevchenko wa Ukraine na Aliaksandr Hleb wa Belarus.

Walotwaa mara tano ni Marek Hamsik (Slovenia), Robert Lewandowski (Poland), Goran Pandev (Macedonia) na mstaafu Kakha Kaladze (Georgia).

Kwenye baadhi ya nchi tuzo za mchezaji Bora wa mwaka zina mifumo tofauti kama vile Portugal ambako zipo za aina mbili za yule achezae Ligi ya ndani na yule achezae nje ya Nchi. 
Huko, kwa wachezaji wa nje, Cristiano Ronaldo amezoa mara nane  katika miaka kumi iliyopita.

Na Argentina wana mfumo wa aina hiyo ingawa kabla haijabaguliwa Lionel Messi alibeba tuzo mara mbili na ilipotofautishwa kati ya wachezaji wa ndani na nje, Messi alipewa mara nane kati ya tisa kwa wa nje tangu wakati huo.

No comments:

Post a Comment