MABINGWA
watetezi Tanzania bara Yanga
wamelazimishwa sare ya bao 1-1 katika mchezo wa 17 wa Ligi Kuu Soka
Tanzania bara dhidi ya African Lyon.
Katika
mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, mabao yalifungwa
na Ludovick Venance wa African Lyon na Amis Tambwe kwa upande wa Yanga.
Sare
hiyo itaendelea kuibakiza Yanga kwenye nafasi ya pili ikifikisha jumla ya
pointi 37 nyuma ya vinara Simba yenye pointi 38.
Matokeo
hayo yana faida kwa Simba kama itashinda mchezo wake wa leo dhidi ya JKT Ruvu
utakaochezwa kwenye uwanja wa Uhuru, itawaacha wapinzani wake kwa tofauti ya
pointi nne kwa kuwa itafikisha pointi 41.
Hata
kama Simba itafungwa au kupata sare yoyote bado itaendelea kuongoza.
African
Lyon ndio ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza dakika 59 lililofungwa na Venance baada ya kupata krosi
nzuri ya Abdallah Mguhi.
Venance
aliingia kipindi cha pili dakika 46 kuchukua nafasi ya Awadh Juma.
Aidha, Tambwe akaisawazishia Yanga dakika ya 74 kwa
kichwa baada ya kupata krosi ya Juma Abdul.
Kipindi
cha kwanza cha mchezo huo kila timu haikuweza kufumumania nyavu ya mwenzake.
Yanga
ilitengeneza nafasi nyingi za kufunga na kushindwa kuzitumia kupitia kwa
Tambwe, Haruna Niyonzima, Vicent Bossou, Thaban Kamusoko, Simon Msuva na
Geofrey Mwashiuya huku Mguhi kwa upande wa African Lyon akikosa pia.
African
Lyon inapata sare ya pili mfululizo na kufikisha pointi 19. Timu hii inazidi
kujiwekea rekodi kwa kuzibana timu tatu zinazoongoza ligi, ikitoka kuilazimisha
Azam FC sare ya bila kufungana na pia, iliifunga Simba bao 1-0 katika mchezo wa
raundi ya kwanza.
Kikosi
cha Yanga kilikuwa na Deogratius Munishi
'Dida', Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Kevin Yondan, Vincent Bossou, Saidi Juma,
Simoni Msuva, Thabani Kamusoko/Obrey Chirwa, Amisi Tambwe, Haruna Niyonzima na
Deusi Kaseke/Emmanuel Martin.
African Lyon; Jehu Youthe, Miraj Adam, Baraka Jaffary, Halfan Twenye, Hamadi Waziri, Hamadi Manzi, Hassan Isihaka, Omary Abdallah, Awadh Juma/Ludovick Venance, Thomas Maurice na Abdallah Mguhi.
African Lyon; Jehu Youthe, Miraj Adam, Baraka Jaffary, Halfan Twenye, Hamadi Waziri, Hamadi Manzi, Hassan Isihaka, Omary Abdallah, Awadh Juma/Ludovick Venance, Thomas Maurice na Abdallah Mguhi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment