Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, December 31, 2016

MAYANJA AFURAHIA SIMBA KUKAA KILELENI HADI 2017


KOCHA msidizi wa Simba, Jackson Mayanja, amesema amefurahishwa kuona timu hiyo inakwenda kuanza mwaka mpya wa 2017 ikiwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu kwa tofauti ya pointi nne dhidi ya mahasimu wao Yanga.

Simba juzi iliifunga Ruvu Shooting ya Pwani bao 1-0, katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru na kufikisha pointi 44 ikiiacha nyuma Yanga nafasi ya pili ikiwa na pointi 40.

Akizungumza na gazeti hili baada ya mchezo huo kumalizika, Mayanja raia wa Uganda, alisema kuanza mwaka wakiwa wanaongoza ligi ni jambo zuri kwani watakachokifanya wakati ligi itakapoendelea ni kuhakikisha wanaendeleza mikakati yao ya kupata ushindi ili kuendelea kubaki kwenye nafasi hiyo hadi mwisho wa msimu.

“Nawapongeza wachezaji pamoja na benchi zima la ufundi unajua ligi imekuwa ngumu sana lakini wachezaji wamekuwa wakipambana kufa kupona na ndiyo maana leo (juzi) tunaelekea kuuanza mwaka mpya tukiwa tunaongoza ligi tunajua bado hatujamaliza kazi, lakini hapa tulipofika panatia matumaini,” alisema Mayanja.

Akizungumzia timu yake kupata ushindi mdogo wa bao moja katika baadhi ya mechi zao, kocha huyo alisema hiyo inatokana na hali ya hewa kubadilika na joto kuwa kali kiasi cha kuwapa tabu wachezaji wao wakati mchezo ukiendelea.

Alisema  kama ingekuwa ni amri yao wangeomba Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, kutoa dakika kadhaa kwa wachezaji kunywa maji kama ambavyo zinafanya baadhi ya nchi Ulaya, kutokana na joto kuwa kali lakini anaamini hilo litakuwa gumu.

Kwa upande wake kocha wa Ruvu Shooting, Malale Hamsini, alisema mchezo ulikuwa mgumu na sababu iliyowafanya kupoteza mechi hiyo ni makosa madogo madogo ya wachezaji wake, lakini wanakwenda kujipanga kuhakikisha wanafanya vizuri mechi zijazo.