Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, December 31, 2016

WAKONGWE WALIOWAHI KUWIKA BANDARI UWANJANI KESHO


WAKALI wa kusakata kambumbu waliowahi kuchezea timu ya Bandari ‘Bandari Veterani’ wanatarajiwa kushuka dimbani kucheza na timu ya Bandari kesho kwenye uwanja wa Bandari Kurasini, Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili jana, mratibu wa mechi hiyo Kenedy Mwaisabula maarufu kama ‘Mzazi’ alisema mchezo huo wa kufungua mwaka 2017 utaanza saa mbili asubuhi na kuwaalika wapenzi wa soka kujionea vipaji.

“Mchezo utakuwa wa kuvutia kwani wakongwe watakuwa na kazi ya kuwafundisha vijana namna ya kucheza soka bila kukimbizana kwani watakuwa wanapipiga pasi moja na kuachia hivyo nawaalika wote kwani hakuna kiingilio,” alisema Mwaisabula.

Kikosi cha Bandari cha zamani kitaundwa na wachezaji Mohamed Hussein ‘Mmachinga’, Salvatory Edward, Salum Sued ‘Kusi’, Waziri Mahadhi ‘Mandieta’, Semmy Kessy, David Beatus, Mudy Pwani, Zuberi Katwila, Gwakisa Mwandambo.

Wengine ni Simon Butte,  Juma Dallo, Jemedari Said, Husein Mataka, Mick Zongela, Peter Nkwera, Ismail Issa, Rajab Kablao na Abdallah Rajab.

 Pia Mwaisabula alisema mchezo huo utakuwa sehemu ya kuwakutanisha wakongwe hao na kubadilishana mawazo, kwani wengi wao inakuwa nadra kuonana baada ya kuachana kwenye soka la ushindani na baadae watashiriki kwenye sherehe ya kukaribisha mwaka itakayofanyika Bandari.