Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, December 31, 2016

BOCCO AFURAHIA USHINDI WA BAO 1-0


MSHAMBULIAJI wa Azam FC, John Bocco amefurahia ushindi wa bao 1-0 walioupata juzi dhidi ya Prisons katika mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Akizungumza na gazeti hili jana Bocco alisema ni faraja kwao na uongozi kwani michezo miwili mfululizo walipata sare kiasi kwamba timu ilishuka kutoka kwenye nafasi ya tatu hadi ya tano lakini anashukuru wamerejea juu tena.

“Timu yetu ni nzuri lakini matokeo ya uwanjani yamekuwa siyo ya kuridhisha sana hivyo ushindi wa bao 1-0 unaleta faraja japo tunatakiwa kupambana ili tuwe bingwa,” alisema Bocco.

Pia Bocco alisema wanakwenda kwenye kombe la Mapinduzi na wanatarajia kurudi na kombe.
Azam watafungua dimba na Zimamoto mchezo utakaochezwa saa kumi alasiri leo kwenye Uwanja wa Amaan.

Azam ambayo ilicheza bila kocha wake Zeben Hernandes aliyefutwa kazi, ilipata bao lake katika dakika ya 40 ya mchezo huo likifungwa na nahodha Bocco kwa shuti kali.
Ushindi huo umeirudisha Azam nafasi ya tatu baada ya kufikisha pointi 30 sawa na Kagera Sugar wakiwazidi kwa uwiano wa mabao.

Simba inaendelea kuongoza ligi ikiwa na pointi 44 huku Yanga ikishika nafasi ya pili na pointi 40.    

No comments:

Post a Comment