Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, December 28, 2016

AZAM YATIMUA BENCHI LOTE LA UFUNDI



AZAM FC imetimua benchi la Ufundi linaloongozwa na kocha Zeben Hernandez kwa kile kilichodaiwa kuwa ni mwenendo mbovu wa timu hiyo tajiri kwenye Ligi Kuu ya Vodacom.

Azam imekuwa ikipata matokeo mabaya ambayo yamepelekea kushika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi huku matumaini ya kuwania ubingwa ama nafasi ya pili yakiwa yamefifia kabisa.

Habari kutoka ndani ya Azam zimesema kuwa tangu jana uongozi wa klabu hiyo ulikuwa na mazungumzo na makocha hao ambapo leo wamefikia makubaliano ya kuvunja mikataba yao.

Inadaiwa kuwa kumetokea na sintofahamu kati ya wamiliki wa timu hiyo hasa upande wa usajili kwa kuwaacha nyota wao bila sababu za msingi akiwemo Jean Mugiraneza ambapo awali ilielezwa kuwa kocha huyo alidai kutokuwa na matumizi naye hivyo aachwe.

Chanzo kutoka ndani ya Azam FC kinasema kuwa kocha wa Majimaji, Kally Ongalla na Hans Pluigm ndio wanaotajwa kuja kushika mikoba hiyo. Kally aliwahi kuifundisha Azam akiwa kocha msaidizi chini ya Stewart Hall pamoja na Josepg Omog na Hans Pluigm ni mkurugenzi wa ufundi wa Yanga.

No comments:

Post a Comment