TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
CHAMA Cha waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA),
kimepokea kwa masikitikio makubwa taarifa za kifo cha Mwenyekiti wa klabu ya
Azam FC na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu, Said
Muhammed Abeid, kilichotokea jana Novemba 7, 2016 alasiri katika Hospitali
ya Aga Khan, Dar es Salaam.
Atakumbukwa na waandishi wa habari
za michezo kutokana na ukaribu wake na wanahabari na alikuwa na ushirikiano wa
kutosha pale alipoombwa kufanya hivyo, alikuwa kiungo kikubwa kwa TASWA kufanikisha
matukio mbalimbali ya udhamini.
TASWA inatoa
pole kwa familia ya marehemu, klabu ya Azam na wanamichezo wote hapa nchini katika kuomboleza kifo cha Mzee Said, huku
tukiwatakia moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu
cha maombolezo.
No comments:
Post a Comment