Mzee Sitta
ambaye ni Mbunge wa zamani wa Jimbo la Urambo lililopo mkoani Tabora amefariki dunia
usiku wa kuamkia leo Novemba 7, 2016 kwenye Hospitali ya Chuo Kikuu cha Technical
iliyopo Munich nchini Ujerumani usiku wa kuamkia leo Novemba 7, 2016.
Rais Malinzi
amesema kwamba Sitta ameacha alama ya ucheshi na upenzi katika michezo hususani
soka kwani enzi zake hakuficha mapenzi yake kwa klabu ya Simba alikokuwa
mwanachama.
Salamu za
rambirambi za Rais Malinzi zimekwenda pia kwa Rais wa Klabu ya Simba, Evance
Aveva, familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki. Amewataka kuwa watulivu
wakati huu mgumu wa kumpoteza Mzee Samwel Sitta na kwamba anaungana nao kwenye
maombolezo.
No comments:
Post a Comment