Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, November 29, 2016

KLABU YA BRAZIL YAANGUKA NA NDEGE HUKO COLOMBIA


NDEGE iliyobeba Watu 81 wakiwemo Kikosi cha moja ya Timu kubwa Nchini Brazil imeanguka wakati ikikaribia Mji wa Medelin huko Nchini Colombia.
Ripoti toka huko zimedai Ndege hiyo ilipata hitilafu za kiufundi kwenye mfumo wake wa umeme na kuanguka eneo la Milimani.
Zipo ripoti zinazodai Watu 6 wamenusurika na ni pamoja na Wachezaji Wawili wa Klabu hiyo ya Brazil iitwayo Chapecoense iliyokuwa ikienda kucheza Fainali ya Copa Sudamericana dhidi ya Timu ya Mji wa Medellin, Atletico Nacional.
Mechi hiyo ya kwanza ya Fainali hiyo ya Mashindano ya Pili kwa ukubwa kwa Klabu huko Marekani ya Kusini ilikuwa ichezwe Jumatano.
Copa Sudamericana ni Mashindano ya Pili kwa ukubwa kwa Klabu huko Marekani ya Kusini na makubwa kabisa huitwa Copa Libertadores.
Shirikisho la Soka huko Marekani ya Kusini CONMEBOL limesema limesimamisha shughuli zote za Soka.
Wacheza hao Wawili wanaoripotiwa kunusurika wametajwa kuwa ni Alan Ruschel na Danilo.
Chapecoense, iliyoanzishwa Mwaka 1973 na kupanda hadi Daraja la juu la Ligi huko Brazil Mwaka 2014, inatoka Mji wa Kusini mwa Brazil Chapeco na ilifika Fainali ya Copa Sudamericana baada ya Wiki iliyopita kuibwaga Klabu ya Argentina San Lorenzo.
Ndege hiyo iliyoanguka imesemwa ni aina ya British Aerospace 146 na ilibeba Abiria 72 na Wafanyakazi 9 ikiwa ni ya Kampuni ya Ndege za Kukodi za Nchi ya Bolivia, Lamia.