Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, November 29, 2016

KESI YA SIMBA DHIDI YA YANGA SASA IMERUDI KAMATI YA KATIBA, SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI

Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ilikutana Jumapili Novemba 27, 2016 kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Bodi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia mashauri manane.
Shauri la 1. Klabu ya Simba dhidi ya Young Africans na mchezaji Hassan Hamis Ramadhani Kessy
Shauri hili sasa limerudi rasmi kwenye meza ya Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji. Kamati iliyoketi chini ya Makamu Mwenyekiti, Mwanasheria Raymond Wawa imekubali shauri hilo kurejea kwenye Kamati yake na imeahidi kutoa maamuzi ndani ya wiki hii.
Shauri la 2. Malalamiko ya Ayoub Nyenzi na wenzake
Shauri hili pia limepangwa kusikilizwa mwishoni mwa wiki hii. Uongozi wa Young Africans, umeagizwa kuleta nyaraka/kesi inayodai kuwa viongozi hao waliofukuzwa uanachama na Mkutano Mkuu wa dharura ama walishiriki au walifungua shauri mahakamani.
Uongozi wa Young Africans, chini ya Kaimu Katibu Mkuu Baraka Deusdedit ulikubali kuwasilisha nyaraka hizo kabla ya kikao kijacho kinachotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii. Wenzake na Nyenzi ni Hashim Abdallah na Salum Mkemi.
Shauri la 3. Klabu ya Simba na Kocha Amatre Richard
Kamati ilijikita kwenye hukumu yake na kuitaka Sekretarieti ya TFF kuandikia Simba kuhusu msimamo wa hukumu iliyotolewa kwa Simba kumlipa kocha huyo.
Shauri la 4. Malalamiko ya Young Africans dhidi ya Kagera Sugar
Wahusika kwenye shauri hili, wameamuliwa kwenda Dar es Salaam mbele ya kikao kitakachoitishwa mwishoni mwa wiki ili kujieleza. Wahusika hao ni Young Africans waliowasilisha malalamiko, Panone FC ya Kilimanjaro, Kagera Sugar pamoja na mchezaji husika ili hatua stahiki zichukuliwe mara baada ya kuwasikiliza.
Shauri la 6. Malipo ya wachezaji Jerry Tegete, Omega Seme na Thabit Mohammed
Kamati iliamua utekelezwa ufanyike kwa Klabu ya Young Africans kuwalipa wachezaji hao kama uamuzi ulivyokwisha kutoka hapo awali. TFF iandikie barua Young Africans kuhakikisha inawalipa.
Shauri la 7. Madai ya Mchezaji Said Bahanuzi dhidi ya Young Africans.
Suala la Bahanuzi limesogezwa mbele basi kwa kwa kuwa halikujadiliwa.
Shauri la 8. Mchezaji Said Hussein Morald

Mchezaji huyo kwa sasa ni huru baada ya yeye na Klabu ya Singida Unitedf kufikia mwafaka kwa barua ambazo waliwasilisha mbele ya kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji

No comments:

Post a Comment