Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, October 21, 2016

MANJI AWAITA WANACHAMA KWENYE MKUTANO WA DHARURA, AKILIMALI KUTINGA




MWENYEKITI wa Yanga, Yusuf Manji amesema mkutano mkuu wa dharura unaotarajiwa kufanyika kesho utakuwa huru na wa haki na kila mwanachama hai atapewa nafasi ya kutoa duku duku lake kabla ya makubaliano kufikiwa.
Akizungumza na wandishi wa habari jana, Manji alisema wanachama wa klabu ya Yanga wametakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo ambao Makao makuu ya klabu Jangwani, Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili masuala mbali mbali likiwemo suala la ukodishwaji wa timu ya Yanga.
"Mkutano utakuwa huru na wa haki kwa kila mwanachama ambaye amelipia kadi yake atapewa nafasi ya kutoa maoni na dukuduku lake kabla ya makubaliano kufikiwa," alisema Manji.
Pia Manji alisema amesikia kwenye vyombo vya habari (siyo gazeti hili) kuwa Katibu wa baraza la wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali kuwa hajalipa ada ya uanachama jambo ambalo linamwondolea sifa ya kuwa mwanachama lakini Akilimali amelithibitishia gazeti hili kuwa yeye ni mwanachama hai kwani kadi yake amelipia mwaka mzima.
Manji alisema baada ya makubaliano hayo ya mkutano mkuu huo kufanyika uwanja wa mazoezi utaanza kujengwa ndani ya siku 90 katika eneo la Gezaulole lililopo Kigamboni kwa mujibu wa mkataba uliosainiwa na kampuni ya Yanga.
Aidha Manji alisema kuhusu suala la kusainiwa kwa mkataba na bodi ya wadhamini dhidi ya kampuni ya Yanga Yetu kila kitu kitajadiliwa kwenye mkutano huo ambapo wanachama wametakiwa kuwahi mapema huku ulinzi ukiwa ni uhakika.
“Kama itaonekana kuna mgongano wa kimaslahi baina yangu na Yanga kwani Yanga yetu ambayo inakodishiwa timu mimi ndio mmiliki na Yanga napo mimi ndio Mwenyekiti basi wanachama wataamua kama naweza kuendelea au nijiuzulu”, alisema Manji
Manji alisema badala ya wanachama kukimbilia kwenye vyombo vya habari kuongea kuhusu masuala ya klabu wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo ili kuchangia kwa manufaa ya Yanga.
Mkutano huu wa dharura unafanyika huku kikuwepo sitonfahamu ya namna mkataba wa ukodishwaji wa klabu ya Yanga kwa kampuni ya Yanga yetu ulivyosainiwa kabla ya kuridhiwa na kamati ya utendaji na baadaye mkutano mkuu.

No comments:

Post a Comment