Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, msimu 2016/17, raundi ya 12 inaendelea kesho kwa michezo sita
ambako mabingwa watetezi Yanga itakuwa mgeni wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa
Kaitaba mkoani Kagera.
Dar es Salaam, katika Uwanja wa Uhuru African Lyon
itakuwa mwenyeji wa Mbeya City ya Mbeya ilihali Mwadui ya Shinyanga itasafiri hadi
Mtwara kucheza na Ndanda FC kwenye Uwanja wa Nang’wanda Sijaona wakati Stand
United itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye mchezo utaofanyika
Uwanja wa Manungu, ulioko Turiani .
Majimaji
itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting ya Pwani kwenye Uwanja wa Majimaji huko
Songea. Michezo yote mitano hapo juu itaanza saa 10.00 jioni kwa saa za Afrika
Mashariki lakini mchezo kati ya Azam FC na JKT Ruvu itaanza saa 1.00 usiku
kwenye Uwanja wa Azam huko Chamazi, Dar es Salaam.
Jumapili
itakuwa ni zamu ya kinara wa ligi hiyo, Simba ambayo itaikaribisha Toto
Africans ya Mwanza kwenye Uwanja wa Uhuru wakati Tanzania Prisons itapambana na
Mbao FC kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Michezo yote
ya Dar es Salaam, mfumo wa kuingia utabaki kuwa ni uleule wa kutumia kadi za
Selcom kununua tiketi za kielekroniki. Viingilio kwenye mechi za Uwanja wa
Uhuru ni 30,000 kwa Jukwaa Kuu (VIP-A), VIP-B na C 20,000 na mzunguko ni 5,000 wakati Kiingilio Uwanja wa Azam ni
10,000 kwa VIP na Mzunguko ni 3,000.
No comments:
Post a Comment